UTAKUJA UJE
Member
- Aug 4, 2020
- 34
- 78
Najitokeza kuchangia japo kidogo juu ya mgombea wa CCM anayeomba Watanzania tumpe miaka mitano ili aoneshe maajabu. HAYA MAAJABU ALIYOONESHA KWA MIAKA MITANO YANATOSHA!
Hata hivyo, Tanzania ni ya Watanzania wote. CCM hawana hatimiliki ya nchi hii kwamba lazima watawale milele.
Maajabu ya kutawala Tanzania kibabe yametosha! Maajabu ya kubana vyombo vya habari yametosha. Maajabu ya kuahidi milioni hamsini kila kijiji halafu zisipelekwe yametosha. Maajabu ya kuongoza bunge kwa remote na kulifanya likoswe meno yametosha.
Maajabu ya kuchota pesa na kuzipangia maamuzi bila kujadiliwa na kupitishwa bungeni, mfano ujenzi wa uwanja wa ndege Chato nk yametosha. Maajabu ya kutumia pesa za msaada wa wahanga wa tetemeko kule Bukoba kujenga miundombinu ya shule za Nyakato nk, yametosha.
Maajabu ya kuwafukuza chuo wanafunzi UDOM ilihali mtangulizi wako Kikwete aliona umuhimu wa wanafunzi wale kupata haki yao ya elimu kwa njia ile, yametosha.
Maajabu ya kutowapandisha madaraja watumishi hususani walimu, kutoongeza mishahara, kutolipa madai yao yametosha.
Maajabu ya kuharibu mahusiano na nchi jirani yametosha. Maajabu ya wanufaika wa bima ya afya kutopata matibabu yanayostahili na kutakiwa kununua baadhi ya dawa, yametosha. Maajabu ya kuvinyima vyama vya siasa uhuru wa kufanya kazi zao kwa mujbu wa Sheria, yametosha. Maajabu ya kuwafukuza kazi watumishi waluolitumikia Taifa hili kwa miaka mingi pasipo kuwalipa stahiki zao yametosha.
MAAJABU, MAAJABU, MAAJABU MENGI MENGI TULIYOSHUHUDIA KATIKA AWAMU YA TANO YAMETOSHAAAAA. Ni muda sasa wa chama kingine kushika hatamu na kuiongoza Tanzania. Nchi hii ni ya wote