Daddo
JF-Expert Member
- Jan 17, 2013
- 1,435
- 1,025
Mimi Daddo mkazi wa Dar es salaam na mtumishi wa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika moja mashirika ya umma yaliyopo.
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikifatilia kwa karibu mwenendo wa siasa za bongo na nimegundua kwamba mchuano hasa wagombea ngazi ya urais ni mkubwa sana.
Nakiri kabisa kwamba nikiwa na akili timamu bila kushawishiwa na mtu yeyote zaidi ya kusikiliza sera za wagombea, kesho asubuhi nitaenda kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa 2020. Kura yangu kwa ngazi ya URAIS naenda kumptia bwana John Joseph Pombe Magufuli.
Najua Kuna watu watatukana wengine watanuna au wengine kunichukulia Kama kada wa Chama cha Mapinduzi, hayo yote kwangu hayana impact so long as nimeruhusu akili yangu kufanyia kazi sera za wagombea huku nikihusianisha na Tanzania ninayoitaka.
Itoshe tu kusema kwamba wagombea wengine siyo kwamba ni wabaya sana au wanasera mbaya sana la hasha, ni kwamba sera zao tu hazijaendana na vile natamani niione baada ya miaka kadhaa.
Hata wewe mwana jamii mwenzangu nakushauri uachane na kumwangalia mgombea kwa mihemuko ya kisiasa Bali mpime kwa kuangalia ungetamani Tanzania iweje unayeona sera zake zinawiana na kile unachotamani kukuona Basi mpe Kura huyo mgombea.
Achana na kusikiliza propaganda za mtandaoni zisizo na mashiko. Na pia achana na dhana ya kwenda kuchagua chama. Pima watu kwa uwezo wao na siyo kwamba anatokea chama gani. Kumbuka chama hakitaongoza Bali mtu. Kama hawezi kuongoza hata awe na chama kizuri vipi ujue tu hataweza kuongoza.
Mwisho niwaombe wale wanaotamani kuona Tanzania inasonga mbele katika maendeleo ya kweli basi waniunge mkono kesho tukampigie kura za kutosha mheshimiwa John Joseph Pombe Magufuli.