Anayetuhumiwa kumbaka, kumchoma binti wa Miaka 17 kisha kusababisha kifo chake, akamatwa

Anayetuhumiwa kumbaka, kumchoma binti wa Miaka 17 kisha kusababisha kifo chake, akamatwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Arusha RPC.jpg
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linamshikilia mtu mmoja aitwaye Emmanuel Charles (25) mkazi wa wilaya ya Arumeru kwa tuhuma za mauaji ya binti mmoja (17) ambaye jina lake limehifadhiwa mkazi wa wilaya ya Arumeru na Mkoani humo.

Akitoa taarifa hiyo leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema mtuhumiwa huyo alitenda tukio hilo Machi 01, 2025 kwa kumjeruhi marehemu na kitu chenye ncha kali na kisha kumbaka.

Kamanda Masejo ameendelea kufafanua kuwa marehemu alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Arusha.

Aidha, amesema upelelezi wa tukio hili unaendelea na pindi utakapokamilika taratibu nyingine za kisheria zitafuata.

Katika tukio lingine Jeshi la Polisi mkoani humo linaendelea kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio la kifo cha mtoto wa miezi 11 jina limehifadhiwa mkazi wa Olasiti Jijini Arusha ambaye alifariki dunia Machi 04 mwaka huu.

SACP Masejo amebainisha kuwa pindi uchunguzi huo utakapokamilika watatoa taarifa zaidi. Aidha Mwili wa marehemu baada ya kufanyiwa uchunguzi na daktari, tayari umekabidhiwa kwa ndugu kwa ajiili ya taratibu za mazishi.

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limetoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu, pia limesema litaendelea kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja na kuwakamata watu wote watakaobainika kujihusisha na uhalifu.
WhatsApp Image 2025-03-06 at 16.13.54_94e85dee.jpg
 
Kijana wa 27 vs Binti wa 17, hii case ichunguzwe vizuri, kuna namna hapo.
 
Kijana wa 27 vs Binti wa 17, hii case ichunguzwe vizuri, kuna namna hapo.
Kuna namna kwenye kesi ya kubaka na kuua? hata kama wangekua wapenzi au kaliwa pesa zake kuna maana gani kama jitu zee la miaka 27 linaenda kukatisha uhai wa binti mdogo wa miaka 17,
hilo shetani linapaswa likatwe katwe kiungo kimoja kimoja kwa siku kadhaa hadi aombe mwenyewe kifo
 
Arusha matukio yamehamia huko baada ya Dodoma

Inasikitisha sana kutoa uhai wa mtu hata iweje ni kosa kubwa sana.
 
Kuna namna kwenye kesi ya kubaka na kuua? hata kama wangekua wapenzi au kaliwa pesa zake kuna maana gani kama jitu zee la miaka 27 linaenda kukatisha uhai wa binti mdogo wa miaka 17,
hilo shetani linapaswa likatwe katwe kiungo kimoja kimoja kwa siku kadhaa hadi aombe mwenyewe kifo
Ni kweli usemacho, ila vizuri uchunguzi zaidi ufanyike na utoe matokeo halali.
 
Nikisema haya yameletwa na CCM mnasema niache siasa
Acha nikae kimya
Ila ukiinyima Jamii Elimu, utaitawala milele
 
Back
Top Bottom