Anayeuza meno ya Tembo anapomlaumu Ngassa!

Hii kitu ya Eddo Kumwembe imeenda shule sana. Taifa letu halina Values kabisa,,,,
 
Eddo kucha zako zitunze maccm hayapendi kukosolewa yanapenda kusifiwa.
 
Edo said:

Ni kweli. Tumekosa dira kama taifa. Hatujui tulipo wala tunapokwenda. Kabla haujamlaumu mwenzako jiulize, wewe unaifanyia nini nchi yako. je wewe Sekta yako ina maendeleo yanayostahili kabla ya kumnyooshea kidole mwingine?
Huwa nawaza sana.

Hapana siyo Tumekosa dira kama taifa....bali viongozi walio wengi wa taifa hili hawajakosa dira( wanazo dira) ila dira wanatumia zilizo feki(fake) kuliongoza taifa.

Eee...! Ndiyo..! Ni dira feki...dira ya ubinafsi uliopitiliza kuwa uuwaji ....dira ya kutorosha/kuiba wanyamapori na mazao yake nchi za kigeni...huku jamii zinazozunguka hifadhi hazifaidi huduma za jamii....Ni dira feki baadhi ya viongozi na watoto wao kufanya biashara ya magendo, kushiriki kukwepa kodi...kuwatumia wasanii...wanafunzi wanaosoma nje ya nchi kubeba na kuuza madawa ya kulevya hapa nchini na nje ya nchi...huku wakijua wanaharibu kizazi cha sasa na kijacho...

Edo..watanzania walio wengi ambao hawapo madarakani na wachache walioko madarakani wanayo dira halisi (siyo feki). Dira halisi ya kuwakomboa watanzania walio wengi. Tatizo hao viongozi walio na dira feki hawataki kabisa dira hii halisi itumike.


Well done Edo...!!
 
Ni Andiko la maana kwa kweli siyo siri ni kweli kuwa watu hatutimizi wajibu wetu halafu tunaishia kulaumu watu wengine ambao nao pia wanatoa lawama zao kwa kundi la watu wengine, kwa misingi hiyo ni kweli kuwa badala ya kutengeneza cheni ya UWAJIBIKAJI tunatengeneza cheni ya LAWAMA.
 


hhaah! MACC wanamajibu hapa,
wansema TUMEJARIBU, TUMEWEZA, TUNASONGA MBELE
 
Yani mods mmemsikiliza yule zezeta mmeleta uzi huku badala ubaki kule siasani au mchanganyiko?

are u mad!!!!!! mbona unamawazo mgando hivyo yale ni mawazo yake na huyu mtu aliepost hii mada ajakosea kabisa but its okay watu kama hamkosekani humu kila jema mnapinga tu
 
Thread imeenda shule sana dah...lakin n mwendelezo tu wa malalamiko next tym inabidi zije thread za nin kifanyike...
 
Sasa ndo nini hivyo?
 
Sisi tunaongoza katka sera, kilimo kwanza
Mkukuta
Mkurabita
Big result now
Division five
Ufaulu usioridhisha aaah nimechoka
 
Mods ondoa ujinga huu! This is a political forum and not otherwise!
Popote hii makala itakapowekwa ni mwafaka kabisa!Ni uchambuzi uliotukuka, anayechukia ameguswa kinamna na ndo lengo lake haswaa!Big up Edo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…