Trust None
JF-Expert Member
- Feb 12, 2018
- 1,260
- 4,419
Sijui ni upofu au ni chuki binafsi na wapinzani. CCM wanatukana 'mabeberu' bila kukumbuka kuwa bila hawa 'mabeberu' hata huo uchumi wa kati tusingefika.
Ni kweli 'mabeberu' wana mabaya mengi walitufanyia na sasa yapo kupitia 'ukoloni mamboleo' lakini CCM hawahawa wamekuwa wakishirikiana na hawa 'mabeberu' katika nyanja nyingi.
Mabeberu hawa hawa ndio hufadhili ARVs, kondomu, dawa za malaria na dawa zingine za magonjwa hatari. Bila wao sijui wangapi wenye watatizo hayo wangekuwa hai.
-'Mabeberu' ndio wanaotoa misaada na mikopo kwa serikali ya CCM
- Mabeberu ndio huleta pesa za kigeni kupitia utalii.
- Mabeberu hawa ndio huchangia bajeti kuu ya serikali.
- Mabeberu hawa ndio wanamiliki na kuendesha migodi Tanzania.
- Mabeberu hawa ndio hufadhili elimu na ikitokea ZITTO akahoji mambo fulanifulani, CCM hawahawa wanawaka.
NB. Yapo mengi yanayofanywa na 'mabeberu' kwa manufaa ya Tanzania, hivyo CCM mje na hoja nyingine.
Kiufupi Tanzania bila 'mabeberu' ingekuwa nyuma sana kimaendeleo kwahiyo wapinzani kuwakumbatia 'mabeberu' wanaendeleza kile kinachofanywa na CCM