Anayezijua shule hizi tafadhali! Kibugumo sec na makurumla sec

Baba mlezi

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2013
Posts
237
Reaction score
48
Kama kuna mtu anayejua mahali shule hizi zilipo anielekeze
1.KIBUGUMO SECONDARY-Inapatikana TEMEKE
2.MAKURUMLA SECONDARY-Inapatikana KINONDONI

Naomba nijulishwe exactly location yake zilipo na nikitokea Ubungo naweza fika namna gani.
Ninajua tu kuwa moja ipo Temeke na Nyingine halmashauri ya kinondoni, Lakini jinsi ya kufika zilipo ndo mtihani kwangu.
 
Makurumla ipo Magomeni mwembechai baba mzazi! kibugumo cjui labda ipo mkoani
 

kibugumo ipo pande za kigamboni so huna budi kuvuka maji mkuu
 
kibugumo ipo pande za kigamboni so huna budi kuvuka maji mkuu
Longtime enzi za nguvukazi watu waliosadikika hawana ajira zinazowaweka mjini walikamatwa na kupelekwa Kibugumu/Gezaulole kuanzisha mashamba mpaka nimekumbuka ule wimbo unaimba "biashara ya njugu na korosho mama haitufai eehee", anyway location ya Kibugumo hiyo hapo

Name of school
Reg no
Ward
Location
KIBUGUMO
S.3296
MJIMWEMA
KIBUGUMO
 

Hahahahahaaa Mkuu ume nifrahisha sana
 
Hahahahahaaa Mkuu ume nifrahisha sana

Kilikuwa kibao cha Urafiki Jazz ukifika Kibugumo embu ulizia maendeleo though najua utaambiwa wanafanyiwa tathimini ili wahamishwe kupisha NEW CITY. Pata mashairi ya urafiki ikiwa kama ni dedication ya kwenda Kibugumo na Gezaulole


[Jembe Na Panga (Gezaulole) - Urafiki Jazz Band]
[Wote]
Baba na mama, Shangazi na Mjomba
Mji hautufai twendeni Gezaulole!
Biashara ya Kahawa na maji ya Barafu
Sasa haitufai twendeni Kibugumo
Songasonga na kijiji, Tegeta na Mwanadilatu
Haya hasa ndio makao ya mwana wa Mapinduzi
Kitambulisho cha Gezaulole ni Jembe na Panga lako!
Hiyo ndiyo Certificate ya mtu mwenye busara
(Chorus)
[Wote]Gezaulole baba, Gezaulole mama ee
[Mmoja]Biashara ya Njugu na Korosho sasa haitufai eee
[Wote]Gezaulole baba, Gezaulole mama ee
[Mmoja]Twendeni Kibugumo na Mwanadilato kwenye makao mapya
[Wote]Gezaulole baba, Gezaulole mama ee
[Mmoja]Gezaulole baba hoo, Gezaulole mama twende
[Wote]Gezaulole baba, Gezaulole mama ee
[Mmoja]Twende eee..........

 

ukifika kigamboni unapanda gari za geza ulole unashuka kituo kinaitwa shule ambapo kuna shule za kibugomo shule ya msing na sekondar na sekondari ya kidete
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…