Anazaa karibia Kila Mwaka Tangia alipokuwa na Miaka 15

Anazaa karibia Kila Mwaka Tangia alipokuwa na Miaka 15

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
2042718.jpg

Susie Christian akiwa na mumewe na waoto wake saba

Mwanamke mmoja wa nchini Uingereza anazaa karibia kila mwaka tangia alipokuwa na umri wa miaka 15, hivi sasa ana umri wa miaka 24 lakini ana jumla ya watoto saba na tayari ana mimba ya mtoto wa nane. Susie Christian mkazi wa mji wa Norwich nchini Uingereza hivi sasa ana umri wa miaka 24 na alianza kuwashangaza wazazi wake wakati alipopata ujauzito wa kwanza alipokuwa na umri wa miaka 15.

Susie aliwashangaza zaidi wazazi wakati huo pale alipokabidhiwa mtoto wake kwa mara ya kwanza baada ya kujifungua na kusema anataka kuzaa watoto wengi zaidi.

Katika miaka tisa Susie amejifungua jumla ya watoto saba na hivi sasa ana mimba ya mtoto wa nane.

Kutokana na kwamba Susie hafanyi kazi na mumewe naye hana kazi, Susie anapokea jumla ya paundi 24,000 ( takribani Tsh. milioni 48 ) kwa mwaka kama msaada wa malezi ya watoto wake hao.

"Watu waache kunisema sana kwakuwa naishi kwa msaada wa serikali, hakuna kazi nzuri duniani kama kuwa mama wa nyumbani" alisema Susie.

Mama huyo kijana alisema kwamba pamoja na kutokuwa na uwezo wa kuwanunulia watoto wake kila kitu wanachokitaka, anaishi maisha ya furaha na watoto wake.


nifahamishe.com
 
wakizaa wabongo mnasema ooooh wanapenda kuzaa ovyo!!tena bongo hata hawana misaada km hiyo,pound 24,000 kwa mwaka!!!
 
kweli anaijua bible huyo..maana tumeambiwa tuzaane tuongezeke..MUNGU ahimidiwe.
 
kweli anaijua bible huyo..maana tumeambiwa tuzaane tuongezeke..MUNGU ahimidiwe.

Asilete zake za kichovu bana.

Kazi ya kuzaa hajaajiriwa nayo yeye pekee, ni jukumu la kila mtu. Hivi kuna

tuzo ya mtu anayezaa zaidi huko uingereza?

Au labda anadhani anaweza kuingia kwenye guiness book of records!

Anyway , ajitahidi kuongezaongeza, huenda akaweza kuingia huko.
 
wacheni kuharibu lugha tangia manaeke nini wapumbavu wakubwa.
 
Huyu ni shujaa,anatakiwa kupongezwa. Na kama ikitokea familia kama hii hapa Tanzania ukimwi hakuna.
 
The United Kingdom had an estimated 7,839,312 women between the ages of 15 and 34 (2001 Census statistics).

If everyone of these women wants to exercise their reproductive rights in a similar fashion for the next 15 years, this will mean the United Kingdom will be adding around 8 million babies every year, doubling it's population in 7 years, and who knows what would be the economic repercussion of this progression alone, forget about the geometric -if not even some more exotic but deadly logarithmic rates- would surely be a recipe for the casebook Malthusian disaster.

Luckily, the British have first hand experience with the predicament of an overpopulated and underresourced economy, most recently in the squalor of 18th and 19th century urban England as most evidenced and documented by the squalid conditions of Dickensian backdrops.I am quite sure this people will employ their sensible chharacter to avoid a similar ocurence, and that this lady is an anomalous idiosyncracy.

Estimate of a simple projection adding 8 million babies yearly to the population of the UK, in 35- 40 years -Malthusian checks aside - the UK would overtake China and India and become the world's most populous country.

Year Population

2008 60
2009 68
2010 76
2011 84
2012 92
2013 100
2014 108
2015 116
2016 124
2017 132
2018 140
2019 148
2020 156
2021 164
2022 174
 
Last edited:
wacheni kuharibu lugha tangia manaeke nini wapumbavu wakubwa.

Sasa we SONARA ndo labda mpubavu, maana unarekebisha kosa kwa kufanya kosa...Huo ndo upumbavu uliobobea!
Angalia hapo kwenye bluu
 
Back
Top Bottom