Elections 2010 Andaeni Kamera zenu kuelekea October 31st, 2010

Elections 2010 Andaeni Kamera zenu kuelekea October 31st, 2010

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
KUELEKEA UCHAGUZI MKUU… Kambi ya upinzani kuwaanika askari watakaoishabikia CCM
Imeandikwa na Shadrack Sagati, Dodoma; Tarehe: 26th June 2010, Habari Leo


KAMBI ya Upinzani Bungeni imesema haitasita kumtaja askari wa aina yeyote ambaye atabainika anakishabikia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na anakisaidia chama hicho kushinda katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Katika taarifa mbili za kambi hizo za Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wapinzani hao walisema watafanya hivyo kwa vile Katiba ya nchi inawakataza askari na wanajeshi kushabikia chama chochote cha siasa.

Msemaji wa Kambi ya Upinzani, Masoud Abdallah Salim (CUF) alisema mazingira ya jeshi bado yanaonekana kujiimarisha kwa kufuata zaidi mipango, sera na mwelekeo wa chama kilichopo madarakani.

“Hili ni kosa, hivyo hali hii inazidi kutupa mashaka kama kweli jeshi letu halitotumiwa na CCM kutimiza mkakati wake wa kuhakikisha inashinda hata kura za wananchi kwa chama hicho zinakuwa hazitoshi,” alisema.

Salim alisema majeshi ya ulinzi na usalama ni ya Watanzania wote bila ya kujali itikadi zao za kisiasa hivyo hayatakiwi kufuata sera za chama chochote bali yanatakiwa kufuata sheria za nchi na mipango yake au sera zake kama majeshi ya nchi bila ya kuegemea upande wowote wa chama cha siasa.

Alisema kambi ya upinzani ina matumaini kuwa mapungufu yaliyotokea miaka iliyopita ya wanajeshi kushabikia na kutumika kuhakikisha kuwa chama tawala kinashinda na hivyo kusahau wajibu wao hayatajirudia katika uchaguzi ujao.

“Kambi ya upinzani inachosema na kuwataka askari wetu wajitahidi kudhibiti hisia zao binafsi za itikadi za siasa zinazoweza kuwapelekea kutumiwa na wale walio kwenye madaraka,” alisema Salim.

Naye Msemaji wa Upinzaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Ibrahim Muhammad Sanya aliwataka polisi wabaki kuwa walinzi wakati wote wa kampeni hadi kufikia siku ya uchaguzi.

Alimtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema asimamie jeshi lake ili wasitokee baadhi ya askari kuwa na utashi wa kisiasa au kutumiwa na baadhi ya viongozi walio na upofu wa demokrasia kutaka kushabikia kundi fulani.

Sanya alisema Watanzania wote lazima waelewe kwamba hiki ni kipindi muhimu kuelekea kwenye uchaguzi mkuu. Alisema hapo ni mahala pa kujipima ni kiasi gani nchi imepea kidemokrasia. Alisema uchaguzi mkuu ujao uwe ni kioo kwa nchi yetu, Afrika na duniani nzima.

Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrance Masha alisema maandalizi katika uchaguzi huo yanakwenda vizuri na wananchi waliotimiza masharti ya kupiga kura wametakiwa kujitokeza kupiga kura bila woga kwani hali ya amani na utulivu itaimarishwa kipindi chote cha uchaguzi.

Alisema Serikali imejizatiti vya kutosha na kwamba wanatarajia kupokea magari 260 mwezi Agosti mwaka huu na tayari askari wamepewa mafunzo na utayari.

Naye Mbunge wa Karatu Dk. Wilbroad Slaa alisema kuna maofisa wachache ndani ya Jeshi la Polisi wanalipaka matope kwa kuamua kukaa kimya hasa wakati vijana wa CCM wanapokiuka taratibu za nchi.

 
Ili nisiwe oftopik ngoja niulize swali kwenye new sred?
 
Back
Top Bottom