Andamaneni

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775


1)Ole wenu ole wenu,ole wenu mthubutu
Nasema shairi yenu,mkileta utukutu
Mtasimulia kwenu,hamsahau katu
Andamaneni muone,jinsi tutavyowafinya.

2)Tunakikosi imara,kuwashinda watukutu
Kweli siyo masikhara,jeshi hili siyo butu
Chezeeni hizi sura,muujue wake utu
Andamaneni muone,jinsi tutavyowafinya.

3)Anaevunyja sheria,Dawa yake ni mtutu?
Amani tukichezea tutashuka chini putu
Kuliko kuangamia bora muende kisutu
Andamaneni muone,jinsi tutavyowafinya

4)Virungu tutatembeza,tutakua kama simba
Hatutowabembeleza,tutakua kama mamba
Ukweli twawaeleza,msidhani hizi pumba
Andamaneni muone,jinsi tutavyowafinya


5)Ataeleta ubishi,sijute kitoku kumba
Nasema kwa maandishi,sa hiyo hatutofumba
Ile wa kuwasha moshi watoka kiyumba yumba
Andamaneni muone,jinsi tutavyowafinya

6)Ole wenu narudia,msiende andamana
Kile kitachotokea,tusije laumiana
Tuifateni sheria,tusije kuumizana
Andamaneni muone,jinsi tutavyowafinya.

7)Sheria bila shututi,hatuwezi sumbuana
Sheria I kwa manati,hapo tutasuguana
Andamana tuje kati,hapo ndipo twajuana
Andamaneni muone,jinsi tutavyowafinya.

SHAIRI-ANDAMANENI
MTUNZI-Idd Ninga, Arusha
iddyallyninga@gmail.com
+255624010160.
 
Hayo matakataka ya kuvunjia milango ya watuhumiwa mnayo mangapi??
 
Maandamano ni haki ya kikatiba, sasa mashairi ya nini? Nadhani wewe mtu wa ajabu! hasara tupu
 
Mbona watanzania wanaandamana kila siku.Kwa ukandamizaji huo???
Andamaneni watanzania jumuiya za kimataifa zipo.



Watanzania daini katiba mpya na tume huru vinginevyo mtapata tabu Sana
 
Hata hawa jamaa wanajua ktakachoendelea tena watakuwa mstari Wa mbele kuandamana na sio kupga risasi
 
Nachokiamini
1.JWTZ muda wote wanakuwa tayari sio kwa sababu ya maandamano hewa.
2.JWTZ ipo kwa ajili ya kuwalinda raia wake na mipaka ya nchi kwa ujumla
3.Hakuna maandamano yoyote hapa tunatoka povu kujadili kitu ambacho hata hakipo
Tuacheni kufanya upotoshaji na kuchafua jeshi kwa mambo ya kijinga na hewa hewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…