Andazi! Kwanini mtu achague andazi?

Andazi! Kwanini mtu achague andazi?

Joined
Dec 19, 2013
Posts
7
Reaction score
0
Katika hali ya kawaida ni ajabu kwa mtu kuamua kuthaminisha andazi na mtu au taasisi. Hata hivyo, kama ambavyo Sheria ya Sababu na Athari (Cause and Effect Law) ya Aristotle (384–322 BC) inavyoeleza; kila kitu hutokea kwa sababu na kila athari huwa na sababu maalumu.

Aristotle anaona kuwa tunaishi katika ulimwengu unaotawaliwa na kanuni na kwamba kila jambo hutokea kwa sababu mahususi bila kujali tunajua au hatujui.

Kwa mantiki hiyo, mtu akisema anachagua andazi badala ya mtu au taasisi fulani basi tujue wazi kuwa kuna sababu mahususi za uamuzi wake. Je tunazijua sababu hizo au hatuzijui? Hilo halibatilishi ukweli kuwa kuna sababu za uamuzi huo.

Msanii wa Bongo Fleva Ibrahimu Mussa almaarufu kama Roma Mkatoliki katika wimbo wake wa hivi karibuni wa 'Nipeni Maua Yangu' anasikika akidai kuchagua andazi badala ya CCM. Msanii anasema hivi:

"Mi sio CCM sio Chadema hili niliweke wazi
Ila ukiweka CCM na Andazi ntachagua Andazi
Simuamini mtawala na mpinzani simsadiki
Maana wanaendelea kukatika huku deejay kauzima Mziki"

Labda Roma anawakilisha kundi la watu ambao kwao CCM si chochote wala si lolote mbele ya andazi. Labda pia Roma anawakilisha kundi la watu ambao hawaiamini CCM na hawawasadiki wapinzani. Pengine ni kweli hawa wote ni watu wenye uchu tu wa madaraka.Vyovyote iwavyo kuna haja ya kujiuliza kwanini watu wakose imani na watawala pamoja na wapinzani wao? Kila jambo lina sababu na athari zake, ni muhimu kuzijua ili kukabiliana na hali hii.

Ni wajibu kujiuliza kwanini mtu achague andazi?

Hata katika maisha ya kawaida ya kijamii siku hizi watu wanachagua andazi badala ya wenza wao

Tukiona mtu anachagua andazi tusiishie kumshutumu na kulalamika bali tujiulize kwanini achague andazi? Tukishazijua sababu tuzishughulikie, katu andazi halitachaguliwa tena.



images%20(17).jpg
 
Kauli Hiyo ya Roma Imesadifu Hali halisi ya Upinzani Nchini Iliyotokea Kwenye Uchaguzi Huu wa SM..

mpinzani anajaribu Kufikiri Ipo siku Ataweza Kuongoza Nchi hii huku system Bado inawakataaa kabisa tena kwa Uwazi ni Upungufu wa Akili Kuendelea kuamini Kuwa Ipo siku Upinzani utaweza kuchukua Nchi ..

Kuamini Huko Ni sawa na Kauli aliyo itaja Roma Kuendelea Kukatika Huku Dj Kauzima Mziki..

Ni wazi kuwa CCM inabidi Ijitafakari kwa Kukosa Imani na Wanachi ila Wa Kujitafakari zaidi ni wapinzani Ambapo kwa sasa Nawaona kama Hawana akili hata Thumni..(Mtanisamehe ila Mmeprove kwamba Hamna Akili kabisa hata robo) kwa kuamua Kushiriki uchaguzi msiotakiwa Kushiriki..

Nina mengi ya Kuongea ila ngoja kwanza Nishushe Mzigo wa Viazi mbatata Lori ndo limeingia Sasa Hivi nipate DEIWAKA yangu
 
Back
Top Bottom