Andika tabia usiyoipenda ya baadhi ya member wa JF

Orketeemi

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
5,063
Reaction score
12,866
Wakuu nimeanzisha huu kwa lengo la kuonyana kuhusu tabia mbovu zinazoonekana kwa baadhi ya member wa jamiiforums.

Naanza mimi.
1. Sipendi kabisa tabia ya baadhi ya members kuingilia na kuvuraga mada za wenzao kwa kuanzisha majibizano yasiohusika na mada iliyopo. mfano unakuta mtu kaanzisha mada yake ya kutafuta mteja wa bidhaa yake au kutafuta kazi au kuomba ushauri juu ya suala fulani, sasa unakuta kuna member wanaanza kuleta mazungumzo ya ajabu yasiyohusika kabisa. Tabia hii ya hovyo.

2. Tabia nyingine inayokera ni kukuta watu wanapoteza muda kudharau miji au mikoa mingine ndani ya nchi kana kwamba dharau zao zinawasaidia chochote.

Je wewe umeona tabia ipi inayokukera jamvini?
 
Mimi sipendi mtu anaanzisha simulizi flani kisha anaingia majukwaa mengine kutyp na wakati ile simulizi analalamika anatohoa neno kwa neno kwa mfano hadithi ya Adili na nduguze.
 
Binafsi hakuna kinachonikera hapa. Naamini kila binadamu yuko tofauti na mwenzake na katika utofauti huu ndimo mna ukamilifu wetu. Hakuna anachoweza kufanya kiumbe huyu aliyejipachika cheo cha uHomo Sapiens kikanishangaza wala kunikera hasa humu mitandaoni !!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…