Zakaria Lang'o
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 2,593
- 2,768
Kamanda Mambosasa, nasikitika kukuandikia andiko hili. Imelazimu kwa sababu ukiwa Polisi unayesimamia usalama wa raia mkoani Dar es Salaam, nilikuona siku ya hukumu ya kesi ya akina Mbowe pale Kisutu. Jinsi ulivyotembea kibabe ukiingia kwenye gari baada ya Wananchi waliokuwa wakifuatilia hukumu ile kukudindia kuondoka pale mahakamani, nilijua ulikuwa unasubiri wakati muafaka ili utende jambo. Pale mahakamani ulishindwa kwa sababu macho ya Dunia yalikuwa pale. Ulikuwa helpless.
Hivyo ukasubiri katika geti la Segerea, watu waliofurahi wakishangilia kumpokea kiongozi wao. Kwako ikawa kero hivyo kuamua kuwavunja mikono na migongo wasichana tena Wabunge wasio na hatia yoyote. Yaani hatia yao ni kufurahi, nawe kumfurahisha mkubwa wako ukaamua kuwafanyia ukatili wa kutisha.
Lakini Ni mkubwa wako yupi anayekutuma kuumiza raia unaopaswa kuwalinda!!? Je, Ni IGP Siro, Mkuu wa Mkoa wa Dar Bashite au Ni Rais Magufuli!!?
Siamini Kama Rais Magufuli amekutuma kwa sababu alikwishakutolea onyo pale ulipoonekana ukinywa chai na Mo. Kama umesahau nikukumbushe: Rais alisikika akisema "Watanzania si wajinga. Wanahitaji kujua ukweli. Nani alimteka Mo. Maana watu wameonekana wakinywa naye chai na hatuelezwi Nini kilitokea!!"
Leo unarudia tendo Kama Lile Lile kwa kudai akina Halima walikuwa wanahatarisha gereza hivyo ukawaamuru askari wako kuwapa kipigo Cha mbwa mwizi!!!? Mbaya zaidi hujatosheka bado unataka wakajibu mashtaka uliyowabambikia!!!? Huu ni ufidhuli wa kutisha. Ni ujeuri ambao hata Kaburu hakuthubutu. Yaani Mambosasa watu wanaokulipa mshahara ndio hao hao unawafanyia kana kwamba wametoka sayari ya Mars!!?
Mtu mmoja aliwahi kuniambia kuwa Polisi ni kazi ya laana, kweli nimeamini kutokana na vitendo vyako Ndugu Kamanda. Yaani unawavunja watu wanaoshangilia na kufurahi kupokea kiongozi wao mikono na migongo halafu unaona ni sawa tu!!?
Tuna maana gani ya kujitawala na kuwa watu huru kwa kuwa na Polisi aina yako!!? Neno langu la mwisho kwako Kamanda ni kuwa, iwapo utaendelea na hiyo kesi ambayo kwa ukweli wa nafsi yako unajua ni ya kubambikiza, Mungu Muumba Mbingu na Nchi atakuchukulia hatua stahiki kwa sababu kazi hiyo alitakiwa aifanye Mhe. Rais, lakini kwa kuwa huwa hakerwi na vitendo hivi,
JEHOVA aliyewaumba Halima Mdee, Esther Bulaya na wenzao atakuchukulia hatua stahiki ili liwe fundisho kwa makamanda wengine wafidhuli wanaodhani tumewapa bunduki ili kuwahalalishia kutuua au kutulemaza. God forbid!! Hatua gani Mungu atakuchukulia Mimi Sijui, Yeye ataamua.
Neno moja nalifahamu kuwa Yeye daima ni Mungu wa wanaoonewa.
Tafadhali msiunganishe Uzi huu na mwingine.