Andiko kwa Mambosasa

Zakaria Lang'o

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
2,593
Reaction score
2,768
Kamanda Mambosasa, nasikitika kukuandikia andiko hili. Imelazimu kwa sababu ukiwa Polisi unayesimamia usalama wa raia mkoani Dar es Salaam, nilikuona siku ya hukumu ya kesi ya akina Mbowe pale Kisutu. Jinsi ulivyotembea kibabe ukiingia kwenye gari baada ya Wananchi waliokuwa wakifuatilia hukumu ile kukudindia kuondoka pale mahakamani, nilijua ulikuwa unasubiri wakati muafaka ili utende jambo. Pale mahakamani ulishindwa kwa sababu macho ya Dunia yalikuwa pale. Ulikuwa helpless.

Hivyo ukasubiri katika geti la Segerea, watu waliofurahi wakishangilia kumpokea kiongozi wao. Kwako ikawa kero hivyo kuamua kuwavunja mikono na migongo wasichana tena Wabunge wasio na hatia yoyote. Yaani hatia yao ni kufurahi, nawe kumfurahisha mkubwa wako ukaamua kuwafanyia ukatili wa kutisha.

Lakini Ni mkubwa wako yupi anayekutuma kuumiza raia unaopaswa kuwalinda!!? Je, Ni IGP Siro, Mkuu wa Mkoa wa Dar Bashite au Ni Rais Magufuli!!?

Siamini Kama Rais Magufuli amekutuma kwa sababu alikwishakutolea onyo pale ulipoonekana ukinywa chai na Mo. Kama umesahau nikukumbushe: Rais alisikika akisema "Watanzania si wajinga. Wanahitaji kujua ukweli. Nani alimteka Mo. Maana watu wameonekana wakinywa naye chai na hatuelezwi Nini kilitokea!!"

Leo unarudia tendo Kama Lile Lile kwa kudai akina Halima walikuwa wanahatarisha gereza hivyo ukawaamuru askari wako kuwapa kipigo Cha mbwa mwizi!!!? Mbaya zaidi hujatosheka bado unataka wakajibu mashtaka uliyowabambikia!!!? Huu ni ufidhuli wa kutisha. Ni ujeuri ambao hata Kaburu hakuthubutu. Yaani Mambosasa watu wanaokulipa mshahara ndio hao hao unawafanyia kana kwamba wametoka sayari ya Mars!!?

Mtu mmoja aliwahi kuniambia kuwa Polisi ni kazi ya laana, kweli nimeamini kutokana na vitendo vyako Ndugu Kamanda. Yaani unawavunja watu wanaoshangilia na kufurahi kupokea kiongozi wao mikono na migongo halafu unaona ni sawa tu!!?

Tuna maana gani ya kujitawala na kuwa watu huru kwa kuwa na Polisi aina yako!!? Neno langu la mwisho kwako Kamanda ni kuwa, iwapo utaendelea na hiyo kesi ambayo kwa ukweli wa nafsi yako unajua ni ya kubambikiza, Mungu Muumba Mbingu na Nchi atakuchukulia hatua stahiki kwa sababu kazi hiyo alitakiwa aifanye Mhe. Rais, lakini kwa kuwa huwa hakerwi na vitendo hivi,

JEHOVA aliyewaumba Halima Mdee, Esther Bulaya na wenzao atakuchukulia hatua stahiki ili liwe fundisho kwa makamanda wengine wafidhuli wanaodhani tumewapa bunduki ili kuwahalalishia kutuua au kutulemaza. God forbid!! Hatua gani Mungu atakuchukulia Mimi Sijui, Yeye ataamua.
Neno moja nalifahamu kuwa Yeye daima ni Mungu wa wanaoonewa.

Tafadhali msiunganishe Uzi huu na mwingine.
 
Achana na Mambosasa, mtu ambaye anasukumwa sukumwa kuongea chochote, na ule mwili anapendezea kweli kusukumwa sukumwa.
Muacheni aendelee kupata Ugali wake, mnataka njia ya kwenda chooni iote nyasi?
 
Achana na Mambosasa, mtu ambaye anasukumwa sukumwa kuongea chochote, na ule mwkli anapendezea kweli kusukumwa sukumwa.
Muacheni aendelee kupata Ugali wake, mnataka njia ya kwenda chooni iote nyasi?
Hivi ni kweli hamuoni chadema walipokosea kauli zenyewe za wabunge eti tulienda kumtoa Mwenyekiti wetu..!

Mfungwa hatolewi gerezani, anaweza kuachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya adhabu ya hukumu. Kuachiwa huru maana yake walitakiwa kusubili atoke ndiyo wakutane pa kukutana waanze kelele zao ila kupeleka mabishano gerezani chadema hili walikosea sana..!

Alafu huruka ya Mdee na Easter Matiko kujibizana na askari lazima utapigwa tu.

Nilifuatilia maelezo ya Afisa Magereza baada ya kuhumiwa walianzisha ubishi dhidi ya taratibu za wafungwa kupimwa afya hivyo walijua fika hawana mahusiano mazuri na askari magereza sasa kilichowapeleka huko ni nini hasa..?

Binafsi ata ningekuwa mkuu wa gereza kwa ujinga huu utakula bakora ingawa za kistaarabu ila ukileta ugomvi lazima uadhibiwe vyovyote vile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bigmind,
Big mind umekuwa tiny mind. Kwani polisi ni nani yeye hata usibishane nae hasa ukiwa mbunge. Labda hujui hadhi aliyokuwa nayo mbunge tiny mind. Wabunge wanao uwezo wa kumuondoa rais madarakani
 
Zakaria Lang'o,
Mimi binafsi kwa imani yangu. Sitaki kuamini kuwa lile ni jeshi la Magereza. Naweza kusema lile ni special division military force. Ktk nchi za kidikteta vionhozi wasiojiamini na waoga huunda vikosi maalum vya maangamizi vinavuolinda maslahi yao.

Kimsingi vikosi hivyo vikiachiliwa tu ni kama Simba au Chui. Havitumii akili wala busara havina uyu wala ibinadamu. Vumeundwa na kulelewa hivyo kuwa vikitoka nje ya mipaka yake( geohraphical teritories) basi kazi yake ni kuua, kutesa na kuleta maafa tu. Vinaundqa na watu wenye Laana. Kufa na kupotea kwao vikosi hivyo ni furaha maana sio binadamu tena.

Hawana dhamiri za kibinadamu vimeundwa kisaikolojia kuamini hivyo. Vinalelewa mazingira ya hovyo ya kuamini ktk anayetoa order na hivyo vinatumia rasilimali nyingi ya fedha na siraha ili kuviridhisha kuendelea kumtumikia mtoa order.

Vikosi hivyo anavyo PK, alikuwa navyo Mobutu( mosusu), M7 anavyo. Alikuwa navyo Kabila na sidhani kama Jpm hanavyo.
 
Hii ndio africa bhana,madaraka ni matamu kuliko roho za binaadam wenzako.

Sent using tecno tochi
 
Hii ndio africa bhana,madaraka ni matamu kuliko roho za binaadam wenzako.

Sent using tecno tochi
Bobwe2
Wanachosahau watawala wetu ni kuwa hakuna utawala, hata kama una nguvu gani za kijeshi uliodumu madarakani milele........

Waulizeni Jeshi la Polisi la Afrika Kusini enzi zie za ubaguzi, walichokiwa wanawafanyia waafrika Kusini weusi, wako wapi hivi sasa?

Hatimaye wali-sureender kutokana na Peoples Power ya waafrika Kusini weusi

Hata Jeshi letu la Polisi ambalo ni dhahiri kwa sasa linawaonea mno wapinzani, na kuwafanya kama wakimbizi haramu, hususani viongozi wa Chadema, watafika mwisho wao na ku-surrender kutokana na nguvu ya Umma
 
bigmind,
Hulka yao siyo kibali cha huyo Mambosasa kuongea uongo kila wakati. Kwa MO nako aliwadanganyeni hivyo hivyo. Yaani taarifa ya ukweli atakayoiongea mambosasa ni inayohusiana na ajali za barabarani tu basi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…