Andiko lisemalo " Kila nafsi itaonja mauti" ni swali na sio jawabu. Wachina wameanza kujibu. Babu zetu walikaribia kabisa kupata jawabu

Haihitajiki utafiti kujua moja ya sifa za kiumbe hai ni kuzaliwa na kufa.

Umesoma shule wewe ? Au tuachane na shule mtaani kwenu watu hawazaliwi na kufa ?
Umeelewa mada yangu lakini?
 
We ndugu una kamba za kutosha
 
Dini zote na mifumo ya dunia iliyotangulia ndio wananafundisha kwamba kifo ni lazima ila Muumba alikusudia tuishia umilele hapahapa juu ya nchi.

Hosea 13:14
Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu.

1Korintho 15:26
Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.

1Korintho 15:51
Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala(kufa) sote, lakini sote tutabadilika,

Mhubiri 3:11
Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.

Hili sasa linawezekana kwakuwa Muumba ametutafuta na ametupata.

Ufunuo 21:1-3
1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari(mfumo wa dunia) tena.

3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
 
Kila nafsi ITAONJA umauti,
Kwenye quraan aliyesema hiyo kauli ana majibu kwa mujibu wa imani ya kiislamu.

Tutaonja umauti kisha tutafufuliwa(kurejeshewa uhai) halafu huku itapita watu wema na wabaya, baada ya hapo hakuna umauti tena, wa peponi ni peponi, na wa motoni ni motoni, hakuna kufa,hakuna kuzeeka wala nini, na kuna aya inazungumzia ngozi kama kipokezi yani mtu anachomwa moto, kisha kwa uwezo wake muumba ngozi inajirudi, unaendelea kuwa moto, maana anajua ukiwa jivu, ama ngozi ikishaungua saana huwezi pata maumivu.

Aya zipo zimenitoka.

Huu ndio mchango wangu wa tafsiri ya kila nafsi ITAONJA umauti.
 
And u actually believe this ? Dini bana yani mtu ana kutisha kuhusu sehemu ambayo hata yeye mwenyewe hajawahi kufika . Unasikia " jehanamu ni hatari sana ndugu zangu bora kusikia tu"
 
And u actually believe this ? Dini bana yani mtu ana kutisha kuhusu sehemu ambayo hata yeye mwenyewe hajawahi kufika . Unasikia " jehanamu ni hatari sana ndugu zangu bora kusikia tu"
Sijaambiwa na mtu, ni imani yangu aya ndio mafundisho ya yule niliyeamua kumuamini.
 
Sijaambiwa na mtu, ni imani yangu aya ndio mafundisho ya yule niliyeamua kumuamini.
Haya bana anyways sisi tunaamini suala la kutafuta na hatimaye kupata teknolojia ya kuishi milele Mungu ameliweka mikononi mwetu wanadamu na kwamba sisi ndio tunao paswa kutegua hicho kitendawili..



Unadhani kipi kitakuwa more interesting kwetu.

A. Kugundua dawa/teknolojia ya kuishi milele tukiwa bado tupo hapa hapa duniani au


B. Mungu kutoa hiyo teknolojia baada ya kifo? Tukiwa nje ya dunia?
 
Hiyo miti ya mababu wa kiafrika ingekuwepo km unavyosema wazungu wangeishaitumia

Mababu wa africa walikuwa wajinga sana ndio maana walitupa utamaduni wao kiurais tu kwa zawadi za kanzu na balagashia
Na imani ilivyo ya ajabu hata uwe prof wa hiyo imani huwezi ku question hili wakati lipo wazi au ndio maji hufuata mkondo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…