Andres Iniesta, kachumbari ya mpira

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
Andrés Iniesta Luján hakuna shabiki wa soka asiyelijua hilo jina kiungo aliyekuwa muhimili wa klabu Barcelona pia na timi yake ya taifa ya Spain.

Barcelona wamepata pengo lengine baada Xavier Hernández Creus kuwaga rasmi May 2015 na kutimukia Qatari club Al Sadd FC ya Qatar. xavi aliyekuwa anasifika kam kiungo kwenye pasi nyingi aliondoka na kumuachia kitamba cha nahodha Andrés Iniesta ambaye ametangaza kuachana na Barcelona msimu huu na kujiunga na Chongqing Dangdai Lifan ya nchini China

Iniesta ameitumikia klabu ya Barcelona kwa miaka 22 akicheza mechi 669 na kushinda makombe 31. Iniesta anatarajiwa kubeba kombe lake la 9 la La liga msumi huu.

Iniesta alijiunga na Barcelona 1996 akitokea Albacete Balompié ya nchini Spain ambapo alitumika timu hiyo kuanzia 1994- 1996.

Iniesta alijiunga na academy ya Barcelona 1996 ila alipandishwa kuchezea team B ya Barca 2001 mpaka 2003 akicheza michezo 54 nakufunga magoli 5.

Iniesta atakumbukwa kwa alichokifanya kwenye mashindano ya klabu bingwa ulaya 2006 pale Barcelona wakiwa nyuma ya Arsenal ya goli 1 na wakaja ibuka na ushindi wa goli mbili ndipo pale Thierry Henry alipo mpachika jina kiungo uyo Iniesta kitabu cha Sana'a 'Iniesta the book of artist.

2009 Barcelona watamkumbuka kwa alichokifanya katika uwanja wa Stanford Bridge dakika za mwisho alipo malizia cross iliyopigwa na Lionel Iniesta na kuipeleka Barcelona finali ya UEFA

mwaka huo huo 2009 wengi walizani atalikosa pambano la fainali dhidi ya Man United baada ya kuumia ila kocha wa Barcelona Pep Guardiola alisema ataanza na kweli yeye ndio alitoa pass ya mwisho kwa Samuel Eto'o na kuiandika Barca goli la kuongoza na Barcelona ikafanikiwa kuchukua makombe matatu kwa msimu mmoja ikiwa ndio Mara yao ya kwanza.

licha ya kufanya vingi katika soka la Spain na Barca Iniesta hakuwai kuchukua tuzo la Balloon D'or anaondoka ila La liga bado ikiwa inamuitaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…