Andres Iniesta vs Xavi Hernandez

Nkajua ni George anachambua. [emoji818][emoji818][emoji818][emoji818]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeandika vyema ila umemkosea adabu Xavi pamoja na sisi wana JF kwenye maeneo haya.
Xavi Hernandez vs Sesc Fabregas
Xavi Hernandez vs Paul Scholes
Xavi Hernandez vs Sneijder

Ni kumkosea adabu na kumdhalilisha Xavi kumlinganisha na Fabregas

Fabregas ni sawa na mtoto wa shule mbele ya Xavi
 
Daemusin ni shida kwenye hizi kazi za uchambuzi.
don katika ubora wako wa kunipaka mafuta kwa nyuma ya chupa..

hivi kweli uandishi huu wa copy and paste nitaweza kuingia kwenye anga za magwiji kama vile mosdef, captain marvelous, m-mbabe, chief-mkwawa, belo, PTER, lembu, king Ngwaba na bila ya kumsahau captain ollachuga.
 
Kila mtu ana vionjo vyake kwenye uandishi, wewe kuna style fulani unayoitumia, inashawishi kuendelea kusoma na mtu kutamani uandike zaidi.

Mkuu huwa najitahidi sana nisipitwe na makala zako kwenye jukwaa lenu.
 
ahsante sana brother (ile mechi yenu na bwana zitto junior ilimalizika vipi?)
teh teh teh

dar-es salaam amani bado ipo?
bwana corona ameshautia mguu mchuzi
 
ahsante sana brother (ile mechi yenu na bwana zitto junior ilimalizika vipi?)
teh teh teh

dar-es salaam amani bado ipo?
bwana corona ameshautia mguu mchuzi

Zitto Junior anajiita mshabiki wa Atletico Madrid, na kwa sababu Atleti walituadabisha kwetu hata unapobishana na mshabiki wa timu iliyokupa kipigo huku na huku inabidi tu utumie diplomacy, maana hachelewi kukumbusha kipigo alichokupa.

Dar ndo kwanza corona imefika. Hatujui hizi wiki mbili zitakuwaje, ngoja tuone.
 
swadakta, kabla ya mechi huwa ameshaandaa mpango wake utakaomuwezesha apate ushindi wa knock out.
ila jamaa ni mjengaji hoja mzuri sana (nilifikiri yupo vizuri kwenye ulimwengu huu wa kibabe tu) kumpe mpaka kwenye sports anasukuma dozi nzito
 
Yuko vizuri sana, sema mimi huwa kuna wale washabiki wanaoshabikia timu kama Tottenham, Atletico, sijui Newcastle, naona ni wajanja wa kukwepa kuchekwa timu ikichemsha. Maana hakuna mtu mwenye muda na hizo timu.

Wanakuwa wamejijengea wigo wa wao kuzicheka zaidi timu kubwa, maana wao hawana cha kupoteza kwenye timu zao, mara nyingi nawakwepa.
 
mara nyingi yanakuwa ni mapenzi ya mdomoni ila moyoni wengi wao hubakiwa na upendo wao.....
sijambo rahisi kuacha kushabikia timu kubwa kwa kigezo cha kufanya vibaya baadae ushabikie timu nyengine iliyo chini kiubora
 
Inaweza kuwa hivyo, ndo hapo huwa naona kama wanatafuta pa kujificha ili kupunguza ile zongwa zongwa ya kishabiki.

Inshort wanakuwa hawana uvumilivu wa kuchekwa timu zao zinapoharibu, wanaona ni bora kukimbia kwa kutaja timu ambazo hatuna muda nazo.

Nawaelewa watu wa namna hiyo.
 
Wewe ndio unajua vizuri

Iniesta ni mzuri Ila Xavi alikuwa ndio mashine ya Barca kupiga dizaini ile ya tiktok passes

Alivyosepa Xavi zile pasi za Barca zikapungua sana mpira wao ukawa hauna ile ladha tuliyopewa pale Uefa final against man u Hadi Fergie akawa anatetemeka[emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…