Anfield katika zama za Soweto Massacre

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
Na *MÖÑTÉLO 10*

Ni Jambo la heri kuendelea kuwa hai mpaka sasa tuko mwanzoni kabisa mwa karne nyingine dunia Nayo haiko nyuma kuacha kujizungusha katika mhimili wake.

Maisha yanaenda kasi sana kuna muda unapomkuta mwanadamu anaringa unaishia tikisa kichwa kwa uchungu na mwisho unabaki unawaza hivi kesho yetu tunaijua kweli.

June 16 mwaka 1976 katika eneo la Soweto ndani ya ardhi ya madiba mauaji ya kikatili zaidi yalifanyika katika ardhi ya nchi hiyo zaidi ya wanafunzi takribani 700 walipoteza uhai ndani ya kipindi kichache yalianza kama masihara ila kadri muda ulivyozidi kwenda mambo yalizidi kuwa mabaya, Mungu azilaze nafsi zote zilizotangulia mbele ya haki katika mauji yale.

Mfululizo wa tukio hili na jinsi lilivyoenda umenifanya niwaze mbali sana katika ulimwengu wetu huu wa sasa wa soka kuna sehemu pamegeuzwa kuwa machinjio tena sio machinjio madogo ila machinjio makubwa .

*"When you Walk Through The Storm don't be afraid of the darkness cz at the end of the darkness there will be the golden sky and the sweet silver song shall be sing that why we say you will never walk alone"* ni baadhi ya mistari ya kusisimua iliyoko katika wimbo maarufu wa club ya Liverpool.

Wimbo Huu unapopigwa katika dimba la anfield hata mzuka wa bill shankly pale katika nyumba yake ya milele huwa unasisimka na kuamka sio yeye tu hata nguli mwenzie sir Bob Paisley naye hutabasamu katika nyumba yake ya milele ni zaidi ya hisia kuweza kuelezea huu wimbo umejaa ujasiri wa aina yake kama huamini huu wimbo basi muulize mwanasoka bora wa dunia mess kuhusu usiku wa tarehe 07/may 2019 atakusimulia vizuri kuhusu huu wimbo.

This Is Anfield ndilo bango ambalo ni bango maarufu sana bango hili liliwekwa na nguli wa timu hiyo na mwalimu bora kabisa katika historia ya club ya Liverpool na mwanzilishi wa misingi yote ya Liverpool Sir Bill shankly.

Kwa sasa spirits ya bill shankly inaishi ndani ya kizazi cha sasa cha Liverpool katika enzi za uhai wake aliulizwa nyumbani kwako ni wapi alijibu jibu moja tu kuwa sina mji mwingine zaidi ya anfield.

Spirits na mzuka wa bill shank ndio uliompa gerrad na wenzake ubingwa wa kimajabu katika usiku wa ulaya mwaka 2005, mbele ya wababe Ac Milan nani hakumbuki come back bora kabisa kuwahi kufanywa katika kombe la ulaya .

Ni mwaka mzima sasa umeisha huku club ya Liverpool ikiwa haijui nini maana ya kufugwa katika dimba la anfield kloop amepageuza anfield kuwa machinjio ndogo kila anayekuja anasikia harufu ya damu kama unabisha waulize barca watakwambia kikichowakuta nafikiri ni zaidi ya mauji ya soweto.

Lionel Messi hataki kupasikia Liverpool ni sehemu ngumu ambayo alishawahi kucheza mpira, ni afadhali ucheze mpira sokoni kuliko kucheza pale Anfield, mashabiki zao muda wote wanapiga kelele utasema wapo soko la soweto chanji

Kelele ambazo ni kama zinawapa nguvu wachezaji wa Liverpool kuzidi kupambana, jezi zao zinanuka harufu ya damu ya vita, alama tatu kwa kila mchezo ulio mbele yao wanajitoa sadaka kuipata.

Ubingwa wa ligi kuu England katika mitaa yao haujatua kwa zaidi ya miaka 30 sasa, ilionekana ni kama laana katika timu yao, ndani ya msimu huu wajitahidi kila hatua kuifuta dhambi hii kwao.

Kucheza na Liverpool kwa sasa tena katika uwanja wao wa Anfield unahitaji kuwa mwendawazimu kiasi, wanapambana mno kuweza kuibadilisha hapana kuwa ndio kwao.

Watu kama Sadio Mane, Trent Arnold, wanapigana sana kuweza kuona heshima inarudi kwao, nguvu kubwa walipata baada ya kufanikiwa kubeba ubingwa wa klabu bingwa ulaya msimu wa 2018/19 kutoka pale kwenye vichwa vyao wanatembea na msamiati wa ndio kila sehemu.

Liverpool ni machinjio kwa sasa, wachezaji wao mioyo yao imebadilishwa na kuwekwa moyo wa bill shankly wanaishi katika maono yake, Bill shankly ndani ya Liverpool hajawahi kushindwa waanamini watashinda.

Mzimu wa bill shankly na Bob Paisley bado vinaishi katika viunga vya anfield pengine wale mashabiki vichaa katika jukwaa la the koop nguvu wanazotumia kuimba kama Wenda wazimu na kutokukata tamaa ndo silaha kubwa ya mafanikio ya Liverpool kwa sasa ilichokifanya Liverpool ya makinda kwa majirani zao everton siku kadhaa nyuma ni salamu tosha ukimuona mtu anakwenda anfield basi waambie ndugu zake waandae msiba kama wa Soweto mascare.

Maana wale mashabiki nguli wa Liverpool The Kops wanamsemo wao mmja tu *"MADE FOR ME AND I WAS MADE FOR LIVERPOOL*"
"YOU WILL NEVER WALK ALONE".I AM MANCHESTER UNITED SUPPORTER

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maskani banda ninalopenda kutizama mpira tuna misemo “mshindi/anaeongoza ana haki ya kutamba awezavyo”
“Ushindi raha”

So kwa sasa hivi liverpool watu wanaweza izungumzia kadri wawezavyo hii ni kutokana na ubora wao pale!

Kwani huko nyuma mbona watu walikuwa wanajipigia pale pale anfield!! Tena ile liver ya kipenzi changu steven GERRARD

Hakuna cha mzuka wa bill shankly wala nini ni kwamba liver sasa hivi iko moto tu! Huo ndio uhalisia
 
Uko sahihi mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msimu uliopita pale anfield mechi ya mwisho ligi dhidi ya wolves washabiki wa liva walilia sana!!!Msimu wa kucheka ndio huu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…