Angalau 3/10 ya rafiki wa rafikiyo wasipokua rafiki zako, rafikiyo si rafiki yako

Angalau 3/10 ya rafiki wa rafikiyo wasipokua rafiki zako, rafikiyo si rafiki yako

Thecoder

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2015
Posts
1,590
Reaction score
4,244
Kimsingi ili watu wawe marafiki ni lazima wawe na vitu mfanano vya kuongelea, kwa maana kama hamna vitu mfanano vya kuongelea ni ngumu kutengeneza ile bond kati yenu kwa maana baada ya Salam mnakua mnaangaliana tu na badala yake kila mmoja anatoa simu yake anaanza kuperuzi peruri ili wakati usonge.

Lakini mkiwa na vitu vya kuongelea hata muda wa kuchezea simu wala hautakuwepo, kwa maana ni story juu ya story hata muda unavyosonga wala hamuuoni ila mnakuja kushtukia tu giza hili hapa na mnaondoka huku kila mmoja akiwa hajaboreka na kutamani maongezi yangeendelea ila wakati tu ndio ukuta.

Nadhani unaelewa ya kwamba watu tunatofautiana kisifa kwenye maeneo kadha wa kadha ila pia hata kwenye eneo hili la urafiki utofauti huo upo.

Kuna watu ambao ni rahisi sana kutengeneza muunganiko wa urafiki na watu wapya wanaokutana nao, ila kuna watu ambao ni shida sana kuweza kutengeneza muunganiko na watu wapya wanapokutana nao.

Sasa mara nyingi watu wenye uwezo wa kutengeneza marafiki wapya kwa haraka ni wale ambao wanauwezo mzuri wa kukeep up na watu kinamna yoyote ambayo itawafanya watu hao wawe comfortable kabisa.

Ni watu washashi na machachari lakini pia wako na uwezo mzuri wa kumsoma mtu kwa haraka na kuelewa anauwezo wa kuwa huru kwenye story zinazohusu mambo gani hasa, kwahiyo kama ni story za mpira atakupeleka upande huo, kama ni story za technology atakupeleka upande huo, kama ni story za mambo ya burudani kwa ujumla wake basi atakupeleka upande huo, kama ni story za siasa atakupeleka upande huo na kadhalika na kadhalika.

Watu wa namna hii huwa ni wafuatiliaji wa karibu Kila kitu kinachoendelea duniani na mara nyingi huwa hawatengenezi urafiki na mtu usio na faida, kwahiyo ni watu wa kupiga hesabu za karibu na zile za mbali kwa maana anakufuata huku akiwa na uhakika ya kwamba huyu asipo nifaa Leo basi atanifaa hata kesho.

Watu ambao ni wagumu kutengeneza marafiki wapya, huwa namna pekee ambayo itawafanya watengeneze marafiki kwa haraka ni muunganiko, wanapokutana na watu ambao wanapenda vile vitu ambavyo hata wao wanavipenda basi hapo ni story zitapigwa za upande huo mwanzo mwisho, watu hawa huwa si waongeaji sana kwahiyo kama unamjua mtu wa hivi na ukamuona anapokutana na mtu mpya ambae ni mfuatiliaji wa yale mambo ambayo hata yeyehuwa anayafuatilia sana basi unaweza ukahisi huyu sio yeye au ukapata mshangao na kujisemea kumbe huyu mtu huwa anaongea hivi.

Sasa mtu machachari ambae anaweza kuungana na kila mtu yaani cha wote huwa anafanya hivyo kwa maslahi yake binafsi mara nyingi ingawa si mara zote (zingatia neno si mara zote) na yule mtu ambae si machachari yaani mtu ambae si muongeaji sana na ni mgumu kutengeneza marafiki wapya huwa anafanya muunganiko na mtu ambae anajua huyu tutakua tunabadikishana mawazo ya hapa na pale kwenye upande huu.

Kwahiyo urafiki wa kweli huwa haupo sana kwa wale watu ambao ni machachari ila huwa wanajiegesha kwa mtu kwa lengo binafsi na akifanikisha lengo lake basi anapotea ila kwa watu wale ambao ni wagumu anapoamua kuwa karibu na wewe ujue huyo anahitaji kweli muwe marafiki na watu wa namna hii huwa urafiki wao si wamashaka mashaka, ukilinganisha na wale watu machachari.

Na ukitaka ujue ya kwamba rafiki yako ni machachari au mtulivu ili uweze kukaa kitaalam kabla hujapigwa tukio kupitia mgongo wa urafiki basi jitahidi uweze kukutana na marafiki angalau watano wa rafiki yako.

Na hii ni kwakua watu huungana kupitia vile vitu common yaani vitu mfanano vilivyopo kati yao na kwa maana hiyo wewe na rafiki yako mmeungana kwakua mnavyo vitu mfanano kati yenu na kwa namna hiyo hiyo rafiki wa rafiki yako na wewe muunganiko wenu hautokua wa shida, inawezekana msiwe na huo muunganiko wa moja kwa moja katika marafiki zake wote ila kati ya mmoja hadi wawili kwenye marafiki zake watano lazima mtakua na mambo ya kuzungumzia yatakayopelekea muweze kuwa marafiki kwa uharaka.

Lakini ukiona Kila rafiki wa rafiki yako unapokutana nae story zake na zako ni ardhi na mbingu ila rafiki yako unamuona anakeep up kwa furaha zote basi kaa ukijua huyo unaehisi ni rafiki yako anawezekana asiwe rafiki yako kwa maana yupo hapo kwa maslahi fulani bila kujali ya sasa au ya baadae.

Rafiki yako akiwa rafiki yako kweli basi rafiki zake yeye lazima wawe rafiki zako kwa asilimia kubwa kwa maana kile ambacho kiliwaunganisha wewe na rafiki yako lazima kwenye rafiki zake wawili watatu kati ya watano atakua ameungana nao kupitia kitu hiko hiko, kwahiyo itafanya iwe rahisi kwako kuweza kuungana nao pia.

Sio unakutana na mtu ambae kila mkitoka kukaa sehemu unakutana na rafiki zake ambao wako interested na vitu tofauti kabisa ambavyo wewe hata kwenye namna ya uchangiaji wa story zao huoni kwa kuanzia, unabaki tu kama bubu au unatikisa tikisa kichwa tu na tabasamu lisilo rasmi huku moyoni ukiwa unaombea muda uende haraka urudi zako home ukatulie, angalau iwe kwa mmoja au wawili ila unakutana na rafiki zake kumi wote hakuna sehemu mnakutana kwenye story zenu, huyo sio rafiki yako.

Chukua hiyo itakusaidia kujiweka mbali na parasite na kufanya mwaka 2025 uwe mwaka ambao watu wote unaowakeep wawe wale ambao wana mlengo chanya na wewe.

Muwe na sherehe njema za mwaka mpya wakuu, tusherehekee kwa amani ili tuweze kumaliza haka kalikizo salama turudi kwenye majukumu yetu tukiwa na nguvu mpya.
 
Hii thread itapata comments chache mnoo, haivutii kusoma
 
Lakini ukiona Kila rafiki wa rafiki yako unapokutana nae story zake na zako ni ardhi na mbingu ila rafiki yako unamuona anakeep up kwa furaha zote basi kaa ukijua huyo unaehisi ni rafiki yako anawezekana asiwe rafiki yako kwa maana yupo hapo kwa maslahi fulani bila kujali ya sasa au ya baadae.
Ni vigumu kukutana na kundi la watu halafu kila kinachoongelewa kiwe na mantiki kwa kila mmoja wao.

Inaweza kuwa mmekutana kujadili ishu ya biashara, mkimaliza hilo ukaona mazungumzo yameelekea kwenye kabumbu, nk, ambayo hujui chochote, suluhisho ni unazama kwenye simu na kuwa bize. Wakirejea kwenye biashara unajumuika tena.

Kinachotakiwa ni kwamba kile unachojua hata kama ni kimoja, ufahamu wako uwe na tija ili uwe wa thamani kwenye hilo kundi.
 
Ni vigumu kukutana na kundi la watu halafu kila kinachoongelewa kiwe na mantiki kwa kila mmoja wao.

Inaweza kuwa mmekutana kujadili ishu ya biashara, mkimaliza hilo ukaona mazungumzo yameelekea kwenye kabumbu, nk, ambayo hujui chochote, suluhisho ni unazama kwenye simu na kuwa bize. Wakirejea kwenye biashara unajumuika tena.

Kinachotakiwa ni kwamba kile unachojua hata kama ni kimoja, ufahamu wako uwe na tija ili uwe wa thamani kwenye hilo kundi.
Yeah kuna nyakati story huwa ni mchanganyiko ila kwenye mchanganyiko huo huo ni rahisi sana kupata bond baina yenu... Kuna story ambazo huwa ni common vitu kama mpira au kuongelea story mbili tatu za warembo ila unakuta mtu ukiondoa hizo story common ile main character yake na yako ni tofauti kabisa.
 
Back
Top Bottom