Angalia aina hii mpya ya nyadhifa

KiuyaJibu

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2007
Posts
848
Reaction score
191
Ewe:
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Shida ambaye pia ni Ofisa Mwandamizi wa Matatizo ya Ghafla;
Waziri wa Mambo ya Nje wa Mawazo na Ushirikiano wa Kimaskini;
Mwekahazina wa Dhambi;
Mratibu wa Uoga;
Rais Mstaafu wa Mapenzi na Udanganyifu wa Hapa na Pale;
Katibu Mkuu wa Madeni;
Balozi wa Vishawishi na Mkuu wa Malengo Yasiyotimia.

Ukiwa kama mmoja wa watu wanaopenda kujishughulisha,nakuuliza ni yupi kati ya hawa mabosi hapo juu,uko tayari kufanya nae kazi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…