Hahaha umesahau hata wahuni wanazeeka?Bado wazee walikuwa na nguvu ya neno na kambi ya wahuni ilikuwa ndiyo inajijenga.
Hawaamini kama wanaiacha nchi, wanadhani wataishi milele.Kweli wanazeeka ila wanaacha nchi katika dhiki na vidonda!.
Nyumba zingine zinayo wazee ila ama wamebweteka ama wamekubali kushikwa masikio na vichenchede ama vitoto vya afu 2.Wazee ni hazina, wazee ni risasi ya mwisho na mzee ni sehemu ya kwenda kujichukulia maarifa.
Leo kama Taifa unaona yanayoendelea, wazee wote muhimu wameteketezwa ili vijana (taifa la kesho) wabaki wenyewe.
Mfano, mzee Nyerere kwa wakati wake aliweza kusema na kuonya kuepusha dhiki, Mkapa na Mwinyi kwa nafasi yake pia alisema.
Leo sijui ni ubinafsi, katiba imeyumba na imetekwa na wahuni leo hakuna mwenye last say ila kukumbatia 'here we're here over'.
Mnyororo ulikatika pale tulipoambiwa na wazee kijana subiri muda wako bado utafika utaingia tu!, umelazimisha kuingia kabla ya muda wako hatimaye ndiyo hiki sasa.
Kuna shimo mbele na hakuna mzee wa kutuambia kama tutatumbukia au tuna uwezo wa kupita!.
😭 Amani iwe nasi.
Wakikubali kwamba muda wao umeisha maana yake waridhike na walicho vuna kipindi chao, kitu ambacho hakiwezekani.Hata kujifunza kuwa alikuwepo mzee JKN hawataki.
Vijizee vya pwani unavijua au unavisikia.! Havijui kitu kinaitwa uzeeWakikubali kwamba muda wao umeisha maana yake waridhike na walicho vuna kipindi chao, kitu ambacho hakiwezekani.
Wao wanataka wafie serikalini, wao ndio washauri wetu linapokuja swala la ajira, wanatuambia tujiajiri.