Angalizo kwa bima ya afya ya Taifa! NHIF

Angalizo kwa bima ya afya ya Taifa! NHIF

Mnasihi

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2013
Posts
7,762
Reaction score
7,100
Hawa vijana mliowaweka kwenye hospitali mbalimbali kuhakiki kadi za bima kwa wagonjwa ni kero kubwa mno.

Naandika haya kwa masikitiko makubwa kwani hawana customer care nzuri na wanauliza maswali ya kijinga Sana yenye kumkerehesha mgonjwa! Mfano wa swali la Leo hii niliulizwa Kama, "hivi nyumbani kwako una kioo Cha kujitazama?"

Umejiona sura yako ilivyo? Kisha akaifunga kadi isitoe huduma hapohapo na kusema hutopata huduma Hadi ubadlii picha!

Hali hii siyo sawa hata kidogo kwani wateja wenye kadi zenye picha za miaka 10 iliyopita muonekano wao wa Sasa ni tofauti kidogo Sana. Kwanini Hawa vijana badala ya kuhoji uwepo wa kioo nyumbani asikuelekeze juu ya kubadili picha?

Itoshe kuwaambia Hawa maboss wa NHIF kuwa, watoe elimu juu ya kubadili picha za zamani ili zifanane na mtu alivyo Sasa na gharama hizo wazibebe wao na siyo kutulipisha sh. 20000/= huku wanatukata pesa zetu kwenye mishahara!

Pia wawape darasa hao vijana wao kwani Kuna siku watapigwa makofi. Niwatake wenye hospitali za binafsi wawaelimishe hao vijana kwani wanawakimbiza wateja wao.
 
Back
Top Bottom