Angalizo kwa mawakala wa mashine za malipo

Angalizo kwa mawakala wa mashine za malipo

cerengeti

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2011
Posts
3,878
Reaction score
1,626
Kila kitu kina faida na hasara zake.Hata hivyo lile lenye hasara nyingi ni vyema kulishtukia mapema ili kusiwepo na mrundikano wa hasara.
Teknolojia za malipo ya kielektronik zimesaidia pakubwa katika kurahisisha kulipwa kwa wenye makampuni na kwa upande mwengine kubanaa matumizi ya muda na shida za kupanga foleni kwa wateja wa makampuni hayo.
Mafundi wa IT wana uwezo wa  kubadili code za html na javascript ili kufanikisha miamala katika namna tofauti.Leo ikawa hivi na baada ya muda ikawa vile.
Mafundi nao kulingana na ubunifu na umahiri wao wa kuzisanifu hizo code hutofautiana.Mara nyingi hukusudiwa kuleta ufanisi lakini mara nyengine huleta zohali katika miamala ya malipo.Matatizo na hasara zaidi za zohali kwa asilimia kubwa huwakumba mawakala wa mashine hizo za malipo.Hata hivyo wengi wa mawakala wa mashine hizi inaonekana huwa wanadhoofishwa na mashine hizo badala ya kuwaneemesha bila kujua.
 Kwa ushahidi wa mawakala tuangalie faida na hasara ya mashine za malipo za makampuni mawili ya aina hiyo,nayo ni Maxmalipo na Selcom.
Maxmalipo ni moja ya makampuni ya awali ya malipo ya kielektronik,lakini ufundi wao mwingi inaonekana ndio wanaoongoza kwa kusababisha hasara za kisirisiri kwa mawakala wao wasiofuatilia kwa makini.Malipo makubwa ya makampuni yote naamini ni kwa ajili ya Luku.
 Kati ya hawa wawili Selcom ina huduma chache lakini pamoja na uchanga wake  ni salama zaidi kutumia mashine zao kuliko Maxmalipo.Tatizo lake mashine zao zina mzunguko mrefu usio wa lazima katika manunuzi ya luku hasa kwa upande wa kuhitajika kuandika namba mbili za siri kwa kila muamala unaofanyika kabla haujatumwa.
 Mashine za Maxmalipo kwa upande wa luku hakuna uchaguzi kama ilivyo kwa selcom katika ujazaji wa nambari ya simu ya mteja au kutokujaza.Mwanzoni utaratibu huu ulipoanza wateja wengi walikuwa na wasiwasi sana kama kwamba wanafanyiwa ujasusi.Sasa wengi wameuzoea lakini wako wanaoacha kununua wanapoulizwa nambari zao za simu.
Madhumuni ya nambari hizo naamini ni katika kutatua tatizo lililokuwepo kabla la msongamano wa kusubiri.Kwamba ikiwa network sio nzuri basi umeme wa mteja utatumwa baadae kwa kutumia nambari hiyo.Hili hata baada ya kueleweka na wengi akini wateja karibu wote hawalipendi na ikitokea huonekana ni mkosi mkubwa.
MASHINE ZA MAXMALIPO NI HATARIÂ
Baada ya muda mrefu wa matumizi hayo,mawakala nao wakioana kimetoka kile kikaratasi cha ahadi ya kutumwa baadae kwanza huguna kwa kujua usumbufu na hatari ya kupoteza fedha inayofuatia.Hicho kikaratasi kina status check ya muamala husika.Kutokana na udogo wake hakitunziki na wakati mwengine hakisomeki.Baadhi ya mawakala hubaki navyo wenyewe badala ya kuwapa wateja na hii  ni nafuu zaidi kwa wakala kuliko kukitoa.
Tatizo linalofuata limegawika sehemu mbili kubwa.Kwanza asilimia kubwa ya ahadi haitekelezwi pengine kwa kufuia mitandao ya simu ambapo wakala huwa hahusiki moja kwa moja.Wateja wenye kuathirika zaidi ni wale wanaowacha nambari za mtandao wa tigo.Pili ni kuwa ahadi hizo haziaminiki.Wakala kwa kutumia status check anaweza akapata jibu la haukufanikiwa lakini ikawa tayari umefanyika.
 Ili kupata matumaini zaidi,ni vyema wakala akajaribu kutoa uzoa la mwisho la mita husika.Bado njia zote mbili zinaweza zikatoa taarifa za kupotosha hasa katika muda mfupi tangu muamala kufanyika.Hatua muhimu ambayo inamuokoa wakala na hasara ni kwa kuangalia salio lake baada ya kufanya muamala uliopita.Iwapo muamala umekata pesa ya wakala hatua hii huonesha upungufu wa salio sawa na thamani ya muamala.
Bahati mbaya mawakala wengi wanaziamini hizi mashine na hawaangalia salio lao mara kwa mara.Hali hii hupelekea kufanya manunuzi kwa mara ya pili wakiamini muamala haukufanikiwa.Kwa upande wao Tanesco na makampuni mawakala wa malipo hawana huruma na utaratibu wa kumshtua wakala muuzaji.
 Bila kuangalia salio unaweza ukapoteza hata zaidi ya laki moja kwa siku bila kujua.Si upande wa Luku tu bali katika malipo mengine pia.Wako mawakala wamebeba kodi ya magari kwa TRA za mwaka mzima kupitia mashine zao.Hata wanapotoa taarifa kunakuwa na kutupiana mpira baina ya Maxmalipo kama wale wahudumu ni wakweli,baina yao na TRA.
Â
Mawakala wengi wamechukua hizi mashine kwa kutaraji kujiongezea kipato lakini kabla hawajafanya upembuzi.Ukweli ni kuwa wauzaji wengi hawapati faida inayofikia laki moja kwa mwezi ingawa wanajituma kwa nguvu kubwa kabisa mchana kutwa.wako wanaopata faida za baina ya laki 3 na tano na wachache zaidi ya laki 5.Hivyo iwapo kuna kuibiwa kisiri siri na mashine kutokana na sababu yoyote wakala anaweza akawa anatoa mtaji wake kulipia hasara hizo.
 Faida kubwa ya mashine hizi ni kwa kuvutia wateja kwenye biashara nyengine.Mtu hawezi kumudu kukodi mlango kwa kukusudia kuuza luku pekee.
Wale mawakala wauzaji wenye mashine hubeba uzito mwengine kupitia mfumo wa ahadi wa Maxmalipo.Wale wanaojulikana nyumba wanazoishi hupata maudhi makubwa kutoka kwa wateja wenye hasira.Wakidai umeme wao bila kutaka kujua tatizo la network humalizia hasira zao kwa kupiga milango ya mawakala kwa mateke na magumi yakifuatiwa na matusi.
 Kwa hali kama hizo baadhi ya mawakala wenye mashine hizo mbili wameamua kuhama maxmalipo na kuhamia selcom ambako mpaka sasa hivi ni network ipo au hapana tu.Wateja wengi wako tayari kuzunguka mji au jiji zima kuulizia luku tu mpaka acute sehemu unayotoka moja kwa moja kuliko kuwekesha fedha yake kwa ahadi ya kutumiwa baadae.
 Mashine za selcom nazo si kwamba ni salama na nzuri kiasi hicho.Nazo pia huwa zinakata fedha kimachomacho jambo linaloshuhudiwa na mawakala wenye kuweka kumubukumbu zao sawa sawa.Wakati mwengine inatokea wakala akafanya muamala halafu akasau na akifuatilia akagundua upungufu.Hili lingepata tiba yake kwa mashine zote kulazimika kuweka utaratibu wa kutoa angalau miamala mitano iliyopita,jambo ambalo halipo.Vyenginevyo kuwe na printer ya pili ndogo yenye kuchapisha au kuonesha fedha inavyopungua hatua kwa hatua angalau kwa ufupi.
Maxmalipo wana wahudu kwa wateja wazuri na wa haraka kam m-pesa jambo ambalo selcom hawana,lakini huduma hii ni kwa gharama ya wakala.Makampuni yote ukiwapigia kulalamika wanaweza wakakukana na kujigamba kwamba tatizo la aina Fulani hasa upotevu hakuna kwao.Hata hivyo ni kujigamba tu.Haiwi benki inatokea miamala ya kusahaulika na ya kupungua na kuzidishiwa.Uzuri ni kwamba kwenye mabenki usuluhishi unakuwa mwepesi mara mteja anapogundua.Hii ni tofauti na makampuni ya malipo ya kielektronik kwa vile mambo mengi ni ya kielekronik yanayoishia hewani .
Haya makampuni yawezekana yangepata mafanikio makubwa kama yangewafanya mawakala wao kama ni sehemu ya familia kwa kutafuata na ikiwezekana kufuata ushauri wao wakiwa ni watu wa karibu wa wahudumiwa na watumiaji wa huduma.Kwa mfano siku mtandao  fulani una matatizo na wao kwa ukaribu wao na makampuni mengine wamefahamishwa, basi wangewatumia ujumbe kuwafahamisha  taarifa hizo ili kupunguza uhangaikaji wao mawakala na wateja kwa ujumla.

Angalizo kwa mawakala wa mashine za malipo.
 
Nikushukuru sana. Maxcom mwanzo hawakuwa ukataji pesa. Leo ni mabingwa. Wamefuta hata taarifa ya kamisheni ili wakala usigundue.
 
Back
Top Bottom