Angalizo la nmb mobile services

Rutakyamilwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2009
Posts
1,871
Reaction score
1,237
wanajamii,
Nimeona niwataarifu WANAJAMII tatizo hili linaloweza kukupata pindi utumiapo NMB mobile kununua say LUKU. Jana nili-login kununua umeme nikapata alert SMS kuwa NOT AVAILABLE, nikajaribu tena kwa mara ya pili nikaambiwa NOT AVAILABLE.
Asubuhi leo nitaangalia salio kwenye akaunt yangu nikakuta wamepunguza kiasi nilichokuwa nimetaka kununua LUKU mara mbili (maana nilijaribu mara mbili). Nikawapigia kuwauliza mbona hela zangu mmekata wakati alert SMS ilikuwa inasema NOT AVAILABLE! Wakasema kuwa kulikuwa na tatizo la SMS. KUMBE WALISHAKATA HELA YANGU. wakaniomba niwape namba yangu ya simu wanitumie namba za LUKU, wakafanya hivyo.

KUWENI MACHO KAMA HIYO ITAKUTOKEA
 
Hakuna ustraabu mimi nilijaribu kununua airtime mara nne na kutofanikiwa baada ya hapo nikafanikiwa. Nilipoend benki statement ikaonyesha kuwa nilikatwa basi nilijaribukupiga simu bila majibu. Niliwaandikia kwa email nikitishia kuwashitaki hawajajibu hadi leo. Sijui ofisi zao ziko wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…