Uhakika Bro
JF-Expert Member
- Mar 29, 2022
- 3,644
- 4,315
Baada ya kutumia muda mwingi kutafiti [kigooglegoole] masuala ya nywele na upara na mambo yanayohusiana na hayo, basi leo nimehamishia udadisi wangu JF.
Katika kupitiapitia baadhi ya nyuzi nimegundua kuna watu hasa kwa kutojua wamekuwa wakishauri vitu kuhusiana na upara katika namna inayokanganya.
Zaidi ya mara moja nimekuta mtu akipendekeza mafuta ya kuotesha/kukuza ndevu kama dawa ya uwalaza.
Ni kitu haiingii akilini maana hata wewe ukivuta picha ya mtu yeyote mwenye uwalaza huwa unakuta ana ndevu nyingi nzuri zinang'aa na zimeshiba! Ni kwa nini!? Ni kwa sababu inasemekana kile kihomoni kinachoharibu nywele kichwani nsicho hichohicho haswaa kinachopendezesha nywele kidevuni!!
Kwa mantiki hiyo basi inakuwa ni ngumu kupata mafuta ambayo hapohapo yakuze ndevu na hapohapo yazuie upara. Sayansi bado inaendelea kuchunguza haya mambo yanaendaje endaje. Hicho kihomoni kinaitwa Dihydrotestosterone [DHT]
Kama kawaida uzi bila kapicha!
Kwa wenye tatizo la upara, na tishio la kupata upara ushauri [kulingana na kinachojulikana hadi sasa] watumie mafuta ya mbegu za maboga yalochanganywa na mnyonyo kupaka kichwani.
Pia wapendelee kutumia/kutafuna mbegu za maboga kama chakula maana tafiti mbalimbali zimeonesha ni kitu nzuri kwa ajili ya kulinda tezi dume na upotevu wa nywele.
Atakayefanikiwa kufanya hivyo atumie kwa miezi mitatu hadi sita kisha atupe mrejesho hapa.