Angalizo: Makonda akiendeleza siasa kwenye maandalizi ya Taifa Stars atawagawa watanzania

Malata Junior

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2011
Posts
3,104
Reaction score
2,550
Heshima kwenu wanajamvi.
Natoa tahadhari kwa TFF na watanzania kwa ujumla kuwa makini na propaganda za kisiasa zinazofanywa na mkuu wa mkoa wa Dsm Paul Makonda kila anapozungumzia maandalizi ya mchezo wa Taifa Stars dhididi ya Uganda.

Makonda anatumia nafasi aliyopewa ya mwenyekiti wa kamati ya maandalizi kumsifia rais na serikali badals ya kuwahamasisha watanzania kuisapoti timu ya taifa.

Natoa angalizo kwa TFF kuacha kuwateua wanasiasa kwenye masuala ya mpira kwani kunawagawa watanzania badala ya kuwaunganisha.
 
Mbona watanzania wameshaliona hilo angalizo kitambo ndio maana huoni mzuka...wamejazana mle wanalumumba watupu..ni bahati mbaya Rais wa TFF nae ni kibaraka wa lumumba na mbaya zaidi hanaga USHAWISHI wowote katika soka letu...kwa walivyokosea kujazana humo kwenye kamati tusitegemee kuona hamasa yoyote au kujaa uwanja jumapili...
 
Kazi kweli kweli.........sijui tulikuwa wapi tangu mwanzo mechi ile ya Lesotho chamazi.....Tz tunapenda sana zima moto na shortcut,saiz tunaomba tushinde eti tunawaombea Lethoto wapigwe...Tz buana
 
mkuu
ukimuona DAB kumbuka ya mkuu wetu wa TFF aliyo yasema pale Arusha baada ya mkutano alipokuwa anamzungumzia Michael Richard Wambura...

then Unganisha dot
 
Tuiombee tu timu yetu ya Taifa ishinde na kufuzu hiyo afcon. Ingawa natambua huo ushindi iwapo utapatikana, tutaambiwa ni kwa sababu ya mafanikio ya mtu fulani pasipo kuwapa heshima wanaostahili (wachezaji na benchi la ufundi). Kila kitu tunatanguliza siasa tu na siyo uzalendo.
 
mimi tayari nimeshakubali kujiunga na kamati ya "saidia Uganda ishinde vs Taifa Stars" kutokana na huu utoto wa hawa walioteuliwa kuhamasisha taifa stars.

hii inatosha kuthibitisha usahihi wa takwimu za UN zinazoi rank Tanzania as one of poorest countries kwenye "happiness index" duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…