- Ilifukuza kazi wafanyakazi 800 bandarini Uingereza kwa mkupuo bila kufuata taratibu
- Iliajiri vibarua toka nje ya Uingereza na kuwalipa ujira mdogo kinyume na sheria
- Manamba na vibarua wa Tanzania wajiandae kulipwa kiduchu
- Hisia: Waingereza wanasema rushwa imeibeba DP World
Outrage at new project for firm behind P&O sackings
DP World has been chosen to run a new freeport, despite having sacked 800 workers without notice last year.
Uamuzi wa kuruhusu mmiliki wa P&O Ferries kushiriki katika mradi mkubwa mpya wa miundombinu umesababisha hasira, baada ya kampuni hiyo kuwatimua kazi wafanyakazi 800 bila taarifa mwaka jana.
DP World imeidhinishwa kusimamia pamoja na bandari huru ya Thames huko Essex, kama sehemu ya mpango wa bandari huru wa Rishi Sunak.
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi lilisema ilikuwa ni "uamuzi mbaya", ambao unawezesha waajiri wengine "kutenda bila kujali". P&O Ferries iliwaachisha kazi mamia ya wafanyakazi wa baharini mwezi Machi 2022 na kuwabadilisha na vibarua wa kigeni waliolipwa chini ya mshahara wa chini kinyume cha sheia. Hatua hiyo ilisababisha hasira na kusababisha miito ya kujiuzulu kwa mkurugenzi mtendaji wa P&O, Peter Hebblethwaite.
Wiki moja baadaye, Bwana Hebblethwaite alikiri mbele ya wabunge kuwa uamuzi huo ulikiuka sheria za ajira. Wakati huo, serikali iliita matendo yaliyowakumba wafanyakazi kuwa "hayakubaliki kabisa". Grant Shapps, ambaye wakati huo alikuwa waziri wa usafiri, alisema sheria itabadilishwa ili kuzuia kampuni kuwaachisha kazi wafanyakazi kwa papo hapo.
Ni angalizo tu.