Pre GE2025 Angelina Mabula atuhumiwa kutengeneza mpasuko CCM, ubadhirifu watajwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Nyanswe Nsame

Senior Member
Joined
Jul 9, 2019
Posts
165
Reaction score
181
ANGELINA MABULA ATUHUMIWA KUTENGENEZA MPASUKO CCM, UBADHIRIFU WATAJWA

Mbunge wa jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula ameingia katika vita kubwa na viongozi wenzake wa Chama cha mapinduzi ccm kutokana na kuendesha genge la vijana wahuni wanaotukana na kuanzisha fujo katika mikutano ya chama hicho.

Angelina ambaye aliwahi kuwa waziri wa ardhi nyumba na makazi, anakabiliwa na tuhuma hizo ikiwemo kununulia vijana simu za mkononi ili kuendesha oparesheni ya kuwatukana viongozi mbalimbali wakitaifa na ndani ya mkoa huo.

Sababu zinazochangia mbunge huyo ambaye amekosa mvuto kwa wananchi wake mara kwa mara amekuwa akiitisha mikutano ya hadhara na wananchi kumzomea hususani katika maeneo ya shibula, Nyasaka, kawekamo, Kiseke Ilemela na Mecco na maeneo mengi yenye nguvu jimboni humo.

Inaelezwa kuwa sababu hizo za kukosa mvuto kwa wananchi na kutumbuliwa kwenye uwaziri Angelina ametengeneza chuki kwa viongozi hao wa chama akidai kuwa wanamhujumu na mara nyingi amekosa ushahidi wa namna anavyohujumiwa.

Hata hivyo, wananchi hao kumzomea kunatokana na kushindwa kutatua migogoro ya ardhi katika jimbo la Ilemela kipindi akiwa waziri wa ardhi jambo ambalo limesababisha wananchi kutengeneza chuki dhidi yake na kwa serikali.

Hivyo wananchi wanaeleza kuwa kushindwa kwake kuwasaidia ni moja ya sababu ambazo wanaona hafai kuwa mbunge wao katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na sasa anatumia nguvu kubwa kushawishi viongozi wa CCM na wananchi kurejesha imani.

Jambo lingine linalomtafuna mbunge huyo ni kutuhumiwa kujimilikisha mlima uliopo Igombe ikiwa anafahamu eneo hilo ni la umma pia amechukua maeneo ya wananchi huko Bwiru na kutengeneza hatimiliki feki ili kujimilikisha maeneo hayo.

Maeneo mengine ambayo mbunge huyo amejinufaisha ni katika kata ya Nyamhongolo ambako amejimilisha viwanja mali za wananchi (hatimiliki zipo zinaonesha) kujimilikisha viwanja hivyo kitendo ambacho wananchi wametengeneza chuki kwake na kwa serikali.

Tuhuma nyingine na za muda mrefu ni kutengeneza kampuni feki ya ujenzi iliyojipatia zabuni ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Ilemela akifahamu ni kinyume na taratibu na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya shilingi milioni 500.

Tuhuma nyingine ni kalazimisha kampuni mbili za vinywaji baridi jijini Mwanza kulipa kodi (service levy) kwenye taasisi yake ya Angeline badala ya kwenye akaunti ya halmashauri ya Ilemela akidai kuwa kampuni hizo zimetoa msaada kwa taasisi yake kitendo ambacho ni cha uongo kilichosababisha serikali kupoteza mapato katika Halmashauri hiyo.

Mwiba mchungu kwake ni hatua ambayo sasa chama chake cha mapinduzi nacho kimeona hafai kuwa kiongozi wa wananchi akiwakilisha chama hicho hivyo ni muda sasa wa kutafuta mwakilishi mwingine mwenye ushawishi kwa wanaanchi.

Pia Angelina Mabula, mbali na tuhuma hizo anakabiliwa na tuhuma nyingie ndani ya chama kutengeneza mpasuko mkubwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilemela na mkoa jambo ambalo inadaiwa kuwa mazingira ya kutengeneza safu ya uongozi ndani ya chama hicho.

Sanjali na hilo la kutengeneza mpasuko ndani ya chama, anatuhumiwa kushawishi kuondolewa kwa Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza ili kuandishwa Katibu wa CCM Ilemela Hassan Milanga kushika nafasi ya ukatibu wa mkoa.
 
Hala hala, mti na macho.
Sasa ni mwendo wa kutuhumiana na kuchafuana; Wallah, tutafika Oktoba tukiwa tumechoka!
 
Wanaccm hawaachiani maji ya kunywa mezani- Kikwete
 
Acheni majungu Mama Mhe. Mbunge wetu yuko sawa na hana tatizo na wapigaq kura wake.
 
Utakuwa wewe ni MANGUZO AU umetumwa na manguzo...maana anautafuta ubunge wa ilemela kwa udi na uvumba..
 
ANGELINA MABULA ATUHUMIWA KUTENGENEZA MPASUKO CCM, UBADHIRIFU WATAJWA

Mbunge wa jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula ameingia katika vita kubwa na viongozi wenzake wa Chama cha mapinduzi ccm kutokana na kuendesha genge la vijana wahuni wanaotukana na kuanzisha fujo katika mikutano ya chama hicho.

Angelina ambaye aliwahi kuwa waziri wa ardhi nyumba na makazi, anakabiliwa na tuhuma hizo ikiwemo kununulia vijana simu za mkononi ili kuendesha oparesheni ya kuwatukana viongozi mbalimbali wakitaifa na ndani ya mkoa huo.

Sababu zinazochangia mbunge huyo ambaye amekosa mvuto kwa wananchi wake mara kwa mara amekuwa akiitisha mikutano ya hadhara na wananchi kumzomea hususani katika maeneo ya shibula, Nyasaka, kawekamo, Kiseke Ilemela na Mecco na maeneo mengi yenye nguvu jimboni humo.

Inaelezwa kuwa sababu hizo za kukosa mvuto kwa wananchi na kutumbuliwa kwenye uwaziri Angelina ametengeneza chuki kwa viongozi hao wa chama akidai kuwa wanamhujumu na mara nyingi amekosa ushahidi wa namna anavyohujumiwa.

Hata hivyo, wananchi hao kumzomea kunatokana na kushindwa kutatua migogoro ya ardhi katika jimbo la Ilemela kipindi akiwa waziri wa ardhi jambo ambalo limesababisha wananchi kutengeneza chuki dhidi yake na kwa serikali.

Hivyo wananchi wanaeleza kuwa kushindwa kwake kuwasaidia ni moja ya sababu ambazo wanaona hafai kuwa mbunge wao katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na sasa anatumia nguvu kubwa kushawishi viongozi wa CCM na wananchi kurejesha imani.

Jambo lingine linalomtafuna mbunge huyo ni kutuhumiwa kujimilikisha mlima uliopo Igombe ikiwa anafahamu eneo hilo ni la umma pia amechukua maeneo ya wananchi huko Bwiru na kutengeneza hatimiliki feki ili kujimilikisha maeneo hayo.

Maeneo mengine ambayo mbunge huyo amejinufaisha ni katika kata ya Nyamhongolo ambako amejimilisha viwanja mali za wananchi (hatimiliki zipo zinaonesha) kujimilikisha viwanja hivyo kitendo ambacho wananchi wametengeneza chuki kwake na kwa serikali.

Tuhuma nyingine na za muda mrefu ni kutengeneza kampuni feki ya ujenzi iliyojipatia zabuni ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Ilemela akifahamu ni kinyume na taratibu na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya shilingi milioni 500.

Tuhuma nyingine ni kalazimisha kampuni mbili za vinywaji baridi jijini Mwanza kulipa kodi (service levy) kwenye taasisi yake ya Angeline badala ya kwenye akaunti ya halmashauri ya Ilemela akidai kuwa kampuni hizo zimetoa msaada kwa taasisi yake kitendo ambacho ni cha uongo kilichosababisha serikali kupoteza mapato katika Halmashauri hiyo.

Mwiba mchungu kwake ni hatua ambayo sasa chama chake cha mapinduzi nacho kimeona hafai kuwa kiongozi wa wananchi akiwakilisha chama hicho hivyo ni muda sasa wa kutafuta mwakilishi mwingine mwenye ushawishi kwa wanaanchi.

Pia Angelina Mabula, mbali na tuhuma hizo anakabiliwa na tuhuma nyingie ndani ya chama kutengeneza mpasuko mkubwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilemela na mkoa jambo ambalo inadaiwa kuwa mazingira ya kutengeneza safu ya uongozi ndani ya chama hicho.

Sanjali na hilo la kutengeneza mpasuko ndani ya chama, anatuhumiwa kushawishi kuondolewa kwa Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza ili kuandishwa Katibu wa CCM Ilemela Hassan Milanga kushika nafasi ya ukatibu wa mkoa.
Unamsagia sumu kwa manufaa ya kundi lako ama la nani?
 
Sababu zinazochangia mbunge huyo ambaye amekosa mvuto kwa wananchi wake mara kwa mara amekuwa akiitisha mikutano ya hadhara na wananchi kumzomea hususani katika maeneo ya shibula, Nyasaka, kawekamo, Kiseke Ilemela na Mecco na maeneo mengi yenye nguvu jimboni humo.
Fitna!!
 
Muda wa majungu na kuuana umefika. Ulevi wa madaraka ni mbaya kuliko ulevi mwingine wowote kiwahi kitokea duniani.
 
Back
Top Bottom