Angetile Osia, tunaomba uchambuzi wako udhamini wa GSM kwa Yanga yenye Rais mtumishi wa GSM

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Angetile Osia amekuwa mwepesi sana kujifanya mchambuzi anayepinga kila jema la TFF, TFF wakifanya maamuzi yeye bila kuchelewa hujitokeza kuwapinga.

Angetile amewahi kuwa mtendaji wa TFF, aidha amewahi kuwa mhariri mkuu wa gazeti la Nipashe kwenye kampuni ya The Guardian Ltd pale Mikocheni.

Ni miongoni mwa wasomi wanaoweka sana ushabiki mbele kuliko ukweli halisia.

Leo utopolo inayoongozwa na Rais wake Eng. H ambaye ni mkurugenzi wa uwekezaji pale G..M imeingia mkataba na kampuni ya G...M ambayo Rais wake ni mkurugenzi wa uwekezaji wa G..M.Sote tunajua urais katika vilabu vyetu vya Simba na Yanga sio ajira, Rais wa Simba au Yanga anatakiwa awe na shughuli nyingine nje ya soka, Mhandisi H shughuli yake inayomweka mjini ni G..M, hao hao G..M wameingia makubaliano ya kisheria na Utopolo ambayo Rais wake ni bosi G..M.

Angekuwa Mo Dewji amefanya hivyo Leo kusingekalika humu mitandaoni, Mo dewji aliandika Mo 29 nchi ilichoka kwa maneno, haya yanayoendelea ni sahihi Bw Angetile?

Mbona umekaa kimya sana, unaogopa kumuudhi nani.

Mwisho, nimewahi kusoma mkataba wa Chifu Mangungo wa Msovero vs Dr Karl Peters, someni terms za mkataba wa chifu Mangungo mtakuja kunishukuru, hongereni kwa maendeleo makubwa mnayoyapata Utopolo.

Je, hatuoni tatzo hapa, yaani Rais wa klabu
 
Shida ipo wapi? Umekasirika? Hutaki yanga awe na mkataba na GSM? Ila simba wawe na mkataba na Mbet?
 
Bro dunia hii ukiwa waumia kwa vitu vidogo vidogo utatelekeza familia.
 
Tuliza koo lako wewe huu mchezo autaki hasira, FCC wapo au awapo? Kwaiyo wewe ndo unazo akili nyingiii kuliko tume ya ushindani? Hoja yako ilishakuwa hoja mfu kitambo labda unachojaribu kufanya ni marudio tu ya wakina Shaffi dauda, kina kazumali na wengine wasiojitambua kama wewe, mimi nafikiri ungekuwa mtu wa maana sana kama ungekwenda kufungua mashtaka yako kwenye tume ya ushindani FCC kuliko kubwata hapa autopata msaada wowote ule zaidi ya kupoteza muda na bando lako bure, Na pia uanze na bosi wenu Mo aliyemuweka aliyekuwa mfanyakazi wa makampuni yake kuwa CEO wa klabu na utuambie nafasi za kazi alizitangaza kupitia utaratibu upi mpaka akapatikana uyo babra
 
Udhamini wa GSM Yanga na udhamini wa Mo Simba.. wote magumashi
 
Huyo mjinga naye yuko kwenye payroll ya GSM unataka akate mkono unaomlisha? Kimila zaidi hatuongei wakati wa kula.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Dosari ni ipi au wivu unawasumbua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…