Angola: Visa Vya Kipindupindu Vimeongezeka Hadi 3402 na Vifo 114

Angola: Visa Vya Kipindupindu Vimeongezeka Hadi 3402 na Vifo 114

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Angola imerekodi visa 3,402 vya kipindupindu na vifo 114 tangu mlipuko huo uanze mapema Januari, kulingana na taarifa ya kila siku ya Wizara ya Afya kwa vyombo vya habari jana (Jumanne).

Tangu Februari 1, Angola imekuwa ikiripoti zaidi ya visa 100 vipya vya kipindupindu kila siku, ikifikia kilele cha 295 Februari. 8. Hata hivyo, upimaji wa kimaabara kuthibitisha maambukizi bado ni mdogo, huku kukiwa na takriban sampuli 20 pekee zilizochambuliwa kwa siku.

Tangu kuzuka kwa ugonjwa huo Januari 7, ugonjwa huo umeenea katika majimbo mengi, huku Luanda na mkoa jirani wa Bengo ikiwa ndio imeathirika zaidi.

Zaidi ya watu 925,000 wamechanjwa dhidi ya kipindupindu, ikifikia asilimia 86 ya idadi ya watu, kulingana na jarida la ugonjwa la Wizara ya Afya Jumatatu.
 
Back
Top Bottom