Anguko la Diamond ni sawa na "Mr nice"

Youngblood

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
19,433
Reaction score
56,810
Habari zenu wakuu.

Kwa jinsi upepo unavyovuma sina budi kusema kwamba huyu kijanaa mwenzetu kutoka tandale anaelekea kuanguakia pua kama ilivyotokea kwa msanii mwenzake Mr nice( Lucas mkenda),sababu kubwa itakayofanya huyu kijana wetu aanguke mshindo mkubwa ni kulewa sifa kiasi kwamba anatumia umaarufu wake kutoa nyimbo ambazo hazina viwango.

Kitu kingine ni kwamba inaonekana huyu bwana mdogo anatumia nguvu na ukubwa wa timu yake kusambaza nyimbo ambazo ziko chini ya kiwango kitu ambacho ni makosa makubwa kwasababu sisi ambao hatuna timu au hatuko kwenye timu yake ni rahisi sana kuona ubovu wa nyimbo zake kwasababu tunatumia akili zetu kuchambua tofauti na members wa timu yake ambao hutumia mihemko.

Kitu kingine anachofanya huyu kijana ambacho sio kizuri ni kutumia nguvu kubwa kwenye video ili kuficha ubovu wa audio kitu ambacho kwa upande mwingine kinapelekea kuwanyima haki ya kusikiliza mziki mzuri wale wasiotizama video zake.

Mwisho.
Diamond alikuja vizuri sana lakini huko anakoenda kuna giza nene lisiloelezeka, kwani kwa hizi nyimbo zake mbili mpya za yeye na Neyo na rich mavoko zinaashiria kwamba graph yake inashuka kwa kasi.

Namshauri aangalie sana management aliyonayo kwa sasa maana naona huyu "Salam" anafanya umbeya zaidi kuliko kazi anazotakiwa kufanya,pia ikiwezekana siku moja moja afanye nyimbo zake kwenye studio nyingine siyo kila siku "WASAFI RECORD"maana naamini hawawezi kujua kila kitu,pia aache kufanya vitu kwa mazoeya.
 
Mmmmh kwa kuandika bila hata kupumua, inahashiria unatamani aanguke.

Haya kamsalie ili apae zaidi.
Kijanaa mwenzetu anaelekea shimoni inabidi tumshike shati mapema asije akadumbukia.
 
Diamondi haja anguka

Wimbo na Ne-Yo kwa kweli haukuwa kama ulivodhaniwa utakuwa

Wimbo na Rich Mavoko mimi naona ni mzuri.

Haja anguka, mtu anaye toa nyimbo 5-6 kwa mwaka lazima zisizo kupendeza ziwepo.

Halafu kwa Diamond kuwa kama Mr Nice, hilo ni dua la kuku tu halimpati mwewe asee.
 
Ukiwa na hela aliyonayo mond afu ukafa kibudu ka mr. Nice unahitaji maono na maombi ya lema! mengi ulosema ni sawa ila hiyo ya kusema ataanguka ka mr nice braza umepuyanga mbaya.
Hahaha
Amenikumbusha Lema alivoota Magufuli Mungu kamchukua.

Ni sawa na jamaa hapa, diamond ana weza kufilisika ndio lakini level ya Mr nice hiyo itakuwa balaa
 
Miss Natafuta,
Tatizo hawa team mondi hawataki kusikia wakiambiwa ukweli, ila ngoja tuwaeleze tu wasiposikia basi watajua wenyewe.
 
mbona shigongo kafilisika jamani?
Haa!!
Hilo ndo naliskia now. Ila shigongo hata akifilisika hawezi kufikia kwenye level ya kuwa kapuku kabisa na diamondi akifiliska hawezi kuwa zero kabisa kwani ashajiwekeza tofaut na mr nice

Hivi unafaham mr nice alifilisika vipi, yaan nice alifilisika akawa ana 0 kabsaaa. Na kwasababu mr nice hakuwekeza kwenye asset yoyote. Zaidi alizalisha watoto tuu.
Hakununua hata kuku, kipindi ana hela
 
Mkuu iko hivi hapa double standard hakuna fungia makokoro kama ilivyokuwa kwa chura vinginevyo italeta hisia tofauti kwa wadau maana hii nyimbo haina maaadil kabisa yaan
 
Iceman 3D,
hakuna ajuae kesho mkuu wala hakuna anaemuombea diamond anguko nampenda diamond sana mimi binafsi ila trend yake haipo sawa kama zamani au wewe unasemaje?
 
Mkuu iko hivi hapa double standard hakuna fungia makokoro kama ilivyokuwa kwa chura vinginevyo italeta hisia tofauti kwa wadau maana hii nyimbo haina maaadil kabisa yaan
Utasubiri sana hiyo kitu itokee,kwenye maisha double standard lazima iwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…