Anne Makinda: Wahitimu wanaojitolea watakula shavu kwenye ajira za sensa 2022

Anne Makinda: Wahitimu wanaojitolea watakula shavu kwenye ajira za sensa 2022

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Anne Makinda amesema kwenye ajira za kuhesabu watu kwenye sensa wahitimu ambao hadi sasa wanajitolea sehemu mbali mbali ikiwemo halmashauri watapewa kipaumbele.

WAtakaohesabu watu watakuwa wanatokea katika mikoa husika, yaani hakutakuwa na mtu kutoka Morogoro ambaye ataenda kuajiriwa kuhesabu watu Mbeya, kwa kuwa watu wanakuwa na ufahamu wa maeneo yao zaidi na kuweza kuwafikia watu wengi.

Mama Makinda ambaye ni Kamisaa wa sensa amesema watahitaji watu wengi sana katika zoezi la sensa lakini nafasi za kitaaluma tayari zimeshajaa.
 
Kwa hio watu wasubiri mpaka huo mwaka 2022? Shida zao za mwaka huu na zenyewe zisubiri mpaka mwaka 2022? Matatizo yao pia yasubiri mpaka mwaka 2022? Mikopo yao pia isubiri mpaka mwaka 2022?

Viongozi wetu kweli ni majuha. Ni bora angekaa kimya.
 
Kibarua cha kazi ya Sensa kinasimamiwa Na Halmashaur kazi ipo. Kwenye list ya majina waliombakazi jina la mtu alipo lakini kapata kazi unaanza kushangaa.
 
Na kibarua cha kuhesabu watu kikiisha narudi kujitolea tena daah...

Hizi wanazoziita ajira za kuhesabu watu nazo watazijumuisha kwenye zile ajira milioni 8

Ccm bure kabisa 🚮🚮
 
Anne Makinda amesema kwenye ajira za kuhesabu watu kwenye sensa wahitimu ambao hadi sasa wanajitolea sehemu mbali mbali ikiwemo halmashauri watapewa kipaumbele

WAtakaohesabu watu watakuwa wanatokea katika mikoa husika, yaani hakutakuwa na mtu kutoka Morogoro ambaye ataenda kuajiriwa kuhesabu watu Mbeya, kwa kuwa watu wanakuwa na ufahamu wa maeneo yao zaidi na kuweza kuwafikia watu wengi

Mama Makinda ambaye ni Kamisaa wa sensa amesema watahitaji watu wengi sana katika zoezi la sensa lakini nafasi za kitaaluma tayari zimeshajaa
huyo bibi alishastafu afu amezeeka, anatuletea akili za kizee tu, kwani hakuna vijana wa kusimamia nafasi yake? kwakweli kuna binadam hawarizikagi.

afu eti wanaojitolea ndo wapewe nafasi na huko wanapotijolea ni nani ataendelea kujitolea au nafasi zao zitazibwa na kina nani?

na wanaojitolea kwenye makampuni ya watu binafsi je?

Aache upumbafu wa kifala kuna wahitimu kibao hata kujitolea walikosa, na kuna watu kibao wasio na ajira na kazi, hao ndo walistahili kuwa kipaumbele
 
Dalili ya Kwamba mambo hayapo sawa...

Na hio position itakuwa ya muda gani na package nzima kiasi gani?

Ukiona watu tunagombania particles za ugali badala ya kusonga au kuongeza ugali mwingine ujue kesho yetu tutaanza kunusa tu na kuondoka
 
Hugo bibi amewadanganya mnaojitolea.....



tunazigonga wenye connection katani na halmashauri.


hakuna uchawi.... mpe mtendaji bia 5 kila ukikutana nae.
 
Back
Top Bottom