Anne Makinda amesema kwenye ajira za kuhesabu watu kwenye sensa wahitimu ambao hadi sasa wanajitolea sehemu mbali mbali ikiwemo halmashauri watapewa kipaumbele
WAtakaohesabu watu watakuwa wanatokea katika mikoa husika, yaani hakutakuwa na mtu kutoka Morogoro ambaye ataenda kuajiriwa kuhesabu watu Mbeya, kwa kuwa watu wanakuwa na ufahamu wa maeneo yao zaidi na kuweza kuwafikia watu wengi
Mama Makinda ambaye ni Kamisaa wa sensa amesema watahitaji watu wengi sana katika zoezi la sensa lakini nafasi za kitaaluma tayari zimeshajaa