Anointing with Oil in African Christianity

Anointing with Oil in African Christianity

Aqua

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2012
Posts
1,657
Reaction score
1,231
habari wana jamvi,katika pitapita mitandaoni kutafuta elimu juu ya matumizi ya mafuta ya upako nimekutana na hii.Mtanisamehe ambao lugha ya kiingereza inaweza kuwa shida lakini tuombe uzima kama Mungu akinijaria nialeta somo zuri kuhusu haya mambo kwa lugha ya kiswahili.Soma mwenyewe hapa kama utaweza kusoma ukiwa na biblia yako pembeni ,ubarikiwe.

Na kwa wale ambao huwa hampendi kusoma summary hii hapa chini ila in English

Summary and Conclusion

This study has shown that the biblical motif of anointing with oil for healing is a very popular practice in African Christianity. But a look at the practice of anointing in certain circles of the Nigerian Christian population as reflected above portrays gross perversion(distortion/twisting). It is also absurd theologically to see anointing with oil as a magic fix that makes everything possible.

If biblical anointing is seen as the invocation of the presence and indwelling of the Holy Spirit to work in the life of a believer, it is curious to assume that the Holy Spirit can be so abused to be invoked into a car, a house, electronic equipment, fruit, placenta, application letters, handkerchiefs, real estate, etc., all in the name of religion.

Further, it is also bizarre to emphasize that anointing oil is a remedy for all kinds of diseases. I also believe that the use of anointing oil does not prohibit the use of medication; and even at that the emphasis is to be placed on the prayer of faith as James suggests (James/Yakobo 5:13-16) and also the absolute will of God for such cases.

Whether one uses anointing and medication or only medication, or only anointing, faith should still be emphasized. It is the prayer of faith that saves the sick, for restoration to health includes both physical and spiritual or may involve only physical or spiritual healing.

Kanisa la Nigeria lilipofikia kwa sasa ni shida,tanzania we are not an exception.Hata Tanzania mafuta ya upako yapo na wanayo maandiko yakutetea jinsi wanavyoyatumia.Soma utajifunza kitu.
 
Wakristo wa Africa hawatafuti Maarifa ya kumjua Mungu ila wako busy na uponyaji na miujiza.Unamkuta mtu mzima kabisa Hapendi kujiuliza maswali madogo yeye anaenda mbele tu.Kwa mfano muuza mafuta wa Nigeria Tb joshua alitabiri "eti Hilary clinton atashinda urais""na hakushinda..Hii ni sababu tosha ya kumdisqualify..Yeye ni fake,,mafuta yake ni fake na huduma yake ni fake.

Huyu bwana aliesababisha vifo vya watu hapa Tanzania niliwahi Kusema mtumishi wa Mungu hawezi kujipa aka,,,haitakiwi.
Eti Bulldozer"" Tayari ilitosha kumdisqualify.Yeye ni fake na mafuta yake ni fake.Watu fake wanaojiita watumishi ni watu wanakaribisha kufuru kwa Mungu.

Mwisho nimpongeze Mkuu wa wilaya ya hai Brother Sabaya.Ameongea maneno kuntu.Huyu anafaa awe Mkuu wa mkoa wa dar es salaam ayafungie makanisa ya wachungaji matapeli na wezi waliofanya utauwa kama njia ya kupata faida.

Pia tusisahau chachu ndogo huchachua donge zima,,mchungaji mwenye kashfa ya uzinzi ushirikina,,dhulma watu wanatakiwa wajiulize ni gundi gani imewashikilia ndani ya hilo kanisa lake hawashtuki.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamii hii ya Afrika siyo tu hapa barani Afrika, lakini mahali popote ilipo duniani karibu inasumbuka na mambo yanayofanana ingawa kwa viwango tofauti tofauti.

Hatuwezi kusema miujiza haifanyiki, inafanyika. Lakini ili jambo liweze kufuzu kuitwa muujiza linatawaliwa na sifa fulani.

Sifa inayofanya jambo liwe au liitwe muujiza lazima lidhihirike wazi linapita uwezo wa akili ya binadamu. Jambo hilo lazima lidhihirike wazi wazi kwamba haliwezekani kisayansi au kisaikolojia.

Ukitazama au kuchunguza mambo yanayodaiwa kuwa muujiza utaona ni mambo ambayo yanadhihirika kisayansi au kisaikolojia.

Ajabu ni kwamba mambo ya kisayansi au kisaikolojia yamefanywa kuwa muujiza.

Kuhusu miujiza, kwa kweli haiwezekani nje ya sakramenti au dhamiri safi.
 
Maajabu yanatokana na kazi ya mwanadamu (mysteries are human), ila miujiza ni kazi inayokana na Mungu (miracles are Divine)
 
Back
Top Bottom