kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Anthonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) alilazimika kuyakana matamshi yake kuhusu HAMAS baada ya kulaumiwa na Israel kwa kauli yake kuwa HAMAS ni wapigania ardhi yao iliyokaliwa kimabavu na Israel kwa miaka mingi sasa. HAMAS waliishambulia Israel na kuua wanajeshi wengi wa Israel kama sehemu ya kilio chao ambacho hakuna mtu anaekisikia. Hamas wamenifundisha kuwa ni heri kufia juu ya meza ukipambana na adui mwenye nguvu kuliko kufia uvunguni mwa kitanda kwa njaa ukiwa umejifika kwa kumuogopa adui.
Hamas walijua kuwa Israel ina nguvu kuliko wao na haya yanayotokea sasa yangetokea lakini waliona ni heri ya hivi kuliko vile ambavyo wangenyamaza kama kwamba hana tatizo. Leo hii dunia nzima inawasikiliza na imegawanyika kuhusu vita ya Israel. Na kwavyovyote vile vita hii imekwenda kudhoofisha vita ile ya Ukraine na Urusi kwakuwa undumilakuwili wa dunia na magharibi unaanikwa hadharani.
Hamas ni magaidi kivipi?