MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Bondia Anthony Joshua amefanikiwa kutetea mataji yake ya ubingwa wa dunia WBO,WBA na IBF (world heavyweight titles) kwa kumtwanga bondia aliyeshindikana Mrusi Alexander Povetkin kwa Technical knockout raundi 7.
Bondia Povetkin hakuwahi kupigwa na bondia yeyote ukitoa pambano alilopigwa kwa pointi na Wladimir Klitschko kwenye maamuzi yaliyozua utata mkubwa.
Pambano la AJ na Mrusi huyo halikuwa rahisi kwa raundi tatu za mwanzo ambazo zilishuhudia AJ akiumizwa pua na kuvuja damu. AJ alijirekebisha kuanzia raundi ya nne kwa kuanza kubadili position mara kwa mara huku akishambulia sehemu nyingine ya mwili nje ya kichwa cha Povetkin ambacho ni sugu kwa masumbwi.
Mbinu ya kubadili position na mashambulizi nje ya kichwa cha Povetkin ilionekana kufanikiwa kuanza kumchosha Mrusi huyo na kuzaa matunda raundi ya saba kwa kupokea kipigo mfululizo kichwani na kudondoka chini.
Kocha wa Povetkin alimtaka bondia wake asiendelee baada ya kudondoka lakini Mrusi huyo aliamua kusimama kuendelea kupambana na hii kwa Anthony Joshua ilikuwa ni nafasi nyingine kuonesha kuwa si bingwa wa uzito wa juu wa dunia kwa bahati mbaya kwa kumchakaza vibaya kabla refa Steve Gray hajaingilia kati huku kocha wa Povetkin pia akionesha ishara ya kutaka pambano kusitishwa.
Akihojiwa baada ya Pambano hilo bondia Anthony Joshua amesema yupo tayari kwa pambano lolote mwezi April mwakani na bondia anayemtaka Zaidi ni Deontay Wilder wa Marekani. Anthony Joshua akifanikiwa kukutana na Deontay Wilder na kumshinda atakuwa bingwa wa dunia asiyepigika (undisputed world champion).