Anthony Joshua amtwanga kwa KOs Mrusi Alexander Povetkin

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Bondia Anthony Joshua amefanikiwa kutetea mataji yake ya ubingwa wa dunia WBO,WBA na IBF (world heavyweight titles) kwa kumtwanga bondia aliyeshindikana Mrusi Alexander Povetkin kwa Technical knockout raundi 7.

Bondia Povetkin hakuwahi kupigwa na bondia yeyote ukitoa pambano alilopigwa kwa pointi na Wladimir Klitschko kwenye maamuzi yaliyozua utata mkubwa.

Pambano la AJ na Mrusi huyo halikuwa rahisi kwa raundi tatu za mwanzo ambazo zilishuhudia AJ akiumizwa pua na kuvuja damu. AJ alijirekebisha kuanzia raundi ya nne kwa kuanza kubadili position mara kwa mara huku akishambulia sehemu nyingine ya mwili nje ya kichwa cha Povetkin ambacho ni sugu kwa masumbwi.

Mbinu ya kubadili position na mashambulizi nje ya kichwa cha Povetkin ilionekana kufanikiwa kuanza kumchosha Mrusi huyo na kuzaa matunda raundi ya saba kwa kupokea kipigo mfululizo kichwani na kudondoka chini.

Kocha wa Povetkin alimtaka bondia wake asiendelee baada ya kudondoka lakini Mrusi huyo aliamua kusimama kuendelea kupambana na hii kwa Anthony Joshua ilikuwa ni nafasi nyingine kuonesha kuwa si bingwa wa uzito wa juu wa dunia kwa bahati mbaya kwa kumchakaza vibaya kabla refa Steve Gray hajaingilia kati huku kocha wa Povetkin pia akionesha ishara ya kutaka pambano kusitishwa.

Akihojiwa baada ya Pambano hilo bondia Anthony Joshua amesema yupo tayari kwa pambano lolote mwezi April mwakani na bondia anayemtaka Zaidi ni Deontay Wilder wa Marekani. Anthony Joshua akifanikiwa kukutana na Deontay Wilder na kumshinda atakuwa bingwa wa dunia asiyepigika (undisputed world champion).

1537674010564.png

Yule Mrusi ana speed ya hatari sana. Anthony Joshua angeweza kupoteza pambano hili kirahisi kama asingepigana kwa umakini na kutomsogelea kwa karibu Povetkin lakini pia akisaidiwa na mwili wake mkubwa.
 
Anthony Joshua anaweka rekodi ya aina yake. Akiwa na mapambano 22 tu na umri wa miaka 28 tayari amefanikiwa kuchukua karibia mikanda yote mikubwa ya dunia. Pia amepigana kwa sehemu kubwa na mabondia wagumu na mabingwa wakubwa kwa kipindi kifupi cha professional carrer yake.
 
Bado muingereza mwenzie... Haja cheki nae... Pale lazima akae...
 
Bondia Anthony Joshua amefanikiwa kutetea mataji yake ya ubingwa wa dunia WBO,WBA na IBF (world heavyweight titles) kwa kumtwanga bondia aliyeshindikana Mrusi Alexander Povetkin kwa knockout raundi 7.

Bondia Povetkin hakuwahi kupigwa na bondia yeyote ukitoa pambano alilopigwa kwa pointi na Wladimir Klitschko kwenye maamuzi yaliyozua utata mkubwa.

Pambano la AJ na Mrusi huyo halikuwa rahisi kwa raundi tatu za mwanzo ambazo zilishuhudia AJ akiumizwa pua na kuvuja damu. AJ alijirekebisha kuanzia raundi ya nne kwa kuanza kubadili position mara kwa mara huku akishambulia sehemu nyingine ya mwili nje ya kichwa cha Povetkin ambacho ni sugu kwa masumbwi.

Mbinu ya kubadili position na mashambulizi nje ya kichwa cha Povetkin ilionekana kufanikiwa kuanza kumchosha Mrusi huyo na kuzaa matunda raundi ya saba kwa kupokea kipigo mfululizo kichwani na kudondoka chini.

Kocha wa Povetkin alimtaka bondia wake asiendelee baada ya kudondoka lakini Mrusi huyo aliamua kusimama kuendelea kupambana na hii kwa Anthony Joshua ilikuwa ni nafasi nyingine kuonesha kuwa si bingwa wa uzito wa juu wa dunia kwa bahati mbaya kwa kumchakaza vibaya kabla refa Steve Gray hajaingilia kati huku kocha wa Povetkin pia akionesha ishara ya kutaka pambano kusitishwa.

Akihojiwa baada ya Pambano hilo bondia Anthony Joshua amesema yupo tayari kwa pambano lolote mwezi April mwakani na bondia anayemtaka Zaidi ni Deontay Wilder wa Marekani. Anthony Joshua akifanikiwa kukutana na Deontay Wilder na kumshinda atakuwa bingwa wa dunia asiyepigika (undisputed world champion).

View attachment 874973
Nashangaa huyu myoruba Joshua hajamzidi kale kameiwather utajir.
 
Habari ina upendeleo.
Haielezi Joshua ni Raia wa Nchi ganu zaidi ya kuona mwezie anatoka urusi
Wewe hujui kuwa ni muingereza mwenye asili ya Nigeria... Mama mnigeria na baba kachanganya toka kwa mama mnigeria na baba m-irish...

Rahisi tu nenda Wikipedia kuna taarifa hadi za pambano la mwakani... Nenda kasome
 
Usimulaumu kama hajui
 
Joshua ameonyesha utulivu na kutafuta timming zaidi tangu mwanzo wa mchezo.
Round za mwanzo alikuwa anajisahau anamsogelea mnyama Povetkin ambaye speed na uzito wa ngumi zake ni hatari tupu ...
 
Back
Top Bottom