Anthony Joshua apoteza pambano lake dhidi ya Usyk

Dogo sifa nyingi uwezo hana Afu anataka kupigana na Fury
 
Nakubaliana na hiki ulichosema, Joshua sikuwahi kumuamini kama atadumu kwebye ngumi muda mrefu, jamaa haonekani kuwa true fighter na mengi ya mapambano yake hakuwahi kukutana na mabondia wakali.

Amejidumaza hivyo ndio maana sasa ameanza kukutana na ngumi za moto anapoteza hovyo mapambano, na kusema anapoteza kusudi ili rematch ashinde apige pesa ndefu ni uongo, hawezi chafua rekodi yake kwa kuongeza idadi ya vipigo simply to get more money.
 
AJ siku hizi anapenda biashara kuliko heshima, hapo anatafuta hela ndefu kwenye pambano la marudiano.

Huyo jamaa atachakazwa na AJ kwenye pambano la marudiano hamtaamini.
Siamini kam anaweza kuchafua rekodi yake kwa sababu ya pesa, yaani aongeze idadi ya mapambano ya kupigwa ili apate pesa ndefu, no way kwa professionals.
 
BONDIA wa Ukraine Oleksander Usyk (34) ameshinda pambano la Ubingwa wa Dunia uzito wa juu (heavyweight) na kutwaa mikanda ya WBA, WBO, IBF na IBO kwa kumpiga kwa pointi bondia Anthony Joshua (31) wa England katika pambano la raundi ya 12 lilochezwa katika uwanja wa Tottenham London England, usiku wa kuamkia Jumapili ya 26/09/2021.


Majaji wote watatu walimpa Usyk ushindi kwa pointi 117-112, 116-112, 115-113 , baada ya kichapo hicho Joshua amepoteza mikanda yote minne aliyokuwa anaishikilia.

Pambano hili lilikuwa la 19 kwa Usyk, 13 akishinda kwa KO huku akiwa hajawahi kupoteza hata pambano moja.

Joshua alipanga amtafute Tyson Fury ili wazichape kugombania mkanda wa WBC ambao ni wa uzito wa juu lakini mambo yamebadilika sasa hana mkanda hata mmoja.

Ikumbukwe kuwa Anthony Joshua ndiye mwanadamu pekee aliyewahi beba mikanda minne ya Uzito wa Cruise Weight ndani ya mapambano 15 tu.t
 
Naamini Joshua ataomba Re match na atadundwa tena ashukuru kengele la sivyo Joshua angepigwa KO ya raundi ya 12.
 
Joshua alikuta tu mabondia wa uzito wake wengi wachovu enzi za kina tyson huyu huo ubingwa angeusikia kwenye bomba tu.
 
Hata warudiane mara kumi, AJ awezi kumdondosha USYk, huyo jamaa ni mnyama.
Hii rematch Joshua anaweza asimalize pambano, yule Ruiz alizembea, starehe mingi baada ya kushinda match ya kwanza akachelewa kujiandaa kwa rematch ndio maana akapigwa.
 
Hii rematch Joshua anaweza asimalize pambano, yule Ruiz alizembea, starehe mingi baada ya kushinda match ya kwanza akachelewa kujiandaa kwa rematch ndio maana akapigwa.
Kabisa yani, Luiz alitosha kabisa kumuaibisha AJ, ila Alexander Usyk hanaga huo ujinga, Tony atapigwa mpaka ashangae tena mi naona bora waachie tu hapo hapo maana aibu na kustaafishwa juu😂😂
 
DAVID HAYE aliandika hiki baada ya kipondo cha AJ

Anthony Joshua your world hasn’t crumbled, your bricks remain - a Champion and Warrior it’s time to build again…👊🏽

What a night of heavyweight boxing! 🥳

Tonight Usyk cemented his name in the history books. Unquestionably proving himself to be one of the greatest pound for pounders. He can do no wrong, a great guy in and out of the ring. A truly great story! 🙏🏾

There is a new guy in town and the Heavyweight division just got shaken up once again 👀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…