Mbunge wa Dodoma mjini na waziri wa Madini Mhe. Anthony peter Mavunde ameendelea kuigusa jamii kwa njia nyingi ambapo leo machi 19 , 2025 amesema ataendelea kufanya hivyo ikiwa ni upendo kwa jamii na sio kutafuta ubunge kama watu wengine wasemavyo.
Ameyasema hayo katika hafla ya ugawaji wa vifaa vya masomo kwa watoto waishio mazingira magumu wa shule za msingi zote katika jiji la Dodoma ambapo ametoa madaftari elf 10 mabegi na vifaa vingine vya masomo ili viwasaidie wanafunzi pindi wanapokua masomoni.