Anthony Mtaka anastahili kuongoza tume ya mipango Tanzania

Anthony Mtaka anastahili kuongoza tume ya mipango Tanzania

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Ushauri wangu kwa raisi ni "unahitaji mtu kama Mtaka kuongoza tume ya mipango ndipo uongozi wako utaleta mabadiriko chanya katika jamii"

Shida kubwa ya wataalamu wengi hukimbilia kwenye formula, kanuni n.k lakini hawajui wanatakiwa kuanzia wapi na kuishia wapi.

na kuna watu wako na very good brain, wanajua pa kuanzia na kuishia. yeye akitazama kitu anajua hapa tuko hapa, tukipita pale kesho tumefika kule lakini hawajui kanuni za kitaalamu za kuwafikisha huko. wao ni wachora ramani.

Hii ndiyo brain ya Mtaka, (mkuu wa mkoa wa njembe kwa sasa)

ukitaka kupanga mipango ya maendeleo kwa kutumia wataalamu unashangaa wanatumia formula, kanuni lakini miaka nenda rudi mabadiriko katika jamii hakuna. Labda ukutane na mtaalamu ambaye ana brain kama ya Mtaka alafu akasomea jambo ndiye unakuta anaweza kubuni na kutumia kanuni pia.

Unaweza kutazama ripoti za tume ya taifa ya mipango hata kueleweka hazieleweki, hakuna mpango wowote zaidi ya kutaja vitu obvious ambavyo kila mtu anaweza kutaja.

Lakini ukimsikiliza Mtaka mfano juzi anaongelea kilimo cha ngano njombe mpaka kila mtu anaona yes, mpango wake ni workable, ni mkombozi mkubwa kwa mkoa wa njombe na fursa kwa kila mdau kuanzia vijana, wakulima, wenye mitaji, mabenki, halmashauri, wafanyabiashara wakubwa .

Hivi kwenye planning tunahitaji nini?

Au zile porojo tu za kusema kufikia mwaka 2030 tanzania itafikia uchumi wa kati wa kati bila road map yoyote ya maana ya tunafikaje huko?

Mtaka ana uwezo wa kupima mipango ya wizara yoyote, ana uwezo wa kushauri wizara yoyote, kinachohitajika ni kumpa wataalamu na power ya kusimamia planning, atatufikisha mbali
 
Afrika watu kariba ya kaka Anthony huwa hawafiki mbali, angalia mfano wa yule jamaa mlivyomsagia funza mkampoteza kwa chuki binafsi.
 
Ningeshauri wananchi wangekua wanashirikishwa katika kupanga baadhi ya mipango. Mfano soko la mtaa wananchi watoe mapandekezo ya uwezo wao wa kulipa na huduma wanazohitaji katika soko. Muakilishi wa hawa wananchi atakaa na viongozi wa serikali na wataangalia jinsi budget na uhitaji wa wananchi unavyo uiana.

Kutowashirikisha wananchi kunafanya watu kushindwa kutumia huduma. Unakuta mwananchi anaambiwa kizimba ni laki tatu wakati angeshirikishwa tangu mwanzo angefahamu mapema.
 
Ushauri wangu kwa raisi ni "unahitaji mtu kama Mtaka kuongoza tume ya mipango ndipo uongozi wako utaleta mabadiriko chanya katika jamii...
Mpango upi alioongelea ambao uko Nje ya mipango ya Wazara ya Kilimo na Waziri Bashe?

Si kweli kwamba Wataalamu hawapo Bali kunakosekana utashi wa kisiasa..

Bahati ya Sasa amepatikana Rais ambae anaweza kukubali logic na akatoa pesa harafu aliyeleta proposal akubali kuwajibika in case of anything..

Mfano Bashe alimwambia Rais anaomba Bil.150 Ili ziwe kama dhamana Banks Ili washushe Bei za mbolea,baada ya kujenga hoja na kumshawishi Rais akakubari hilo na amewataka wahusika mbolea ziende Kwa wakulima kweli na si vinginevyo..
 
Mpango upi alioongelea ambao uko Nje ya mipango ya Wazara ya Kilimo na Waziri Bashe?

Si kweli kwamba Wataalamu hawapo Bali kunakosekana utashi wa kisiasa..

Bahati ya Sasa amepatikana Rais ambae anaweza kukubali logic na akatoa pesa harafu aliyeleta proposal akubali kuwajibika in case of anything..

Mfano Bashe alimwambia Rais anaomba Bil.150 Ili ziwe kama dhamana Banks Ili washushe Bei za mbolea,baada ya kujenga hoja na kumshawishi Rais akakubari hilo na amewataka wahusika mbolea ziende Kwa wakulima kweli na si vinginevyo..
Siyo Kila kitu ni mipango.

Inabidi ujenge uwezo wa kuchambua na kujua mpango mzuri ni upi ndipo utaweza kubainisha nani anajua kupanga.

Nichukulie mfano wako wa ruzuku ya mbolea, haya ndiyo mambo ambayo wataalamu wanaibuka nayo wakiambiwa kupanga maana haya ndiyo yanapatikana darasani. Kwangu mimi sioni planning yoyote katika hilo. Ni mambo yenye sura za kutafuta populity lakini haiwezi kubadirisha hali ya kilimo nchini kwa sasa.

Miaka 10 ijayo tunaweza kuwa na haya mambo ya ruzuku na kilimo kikawa ni kilekile au kimekua kidogo sana.

naomba nikushirikishe mpango niliousikia Anthony Mtaka akiusema ambao umenishawishi kuandika mada hii.

nimemsikia akiwaambia watu wa mufindi kwamba waandae programu ya kilimo cha ngano, watenge mashamba na kutangaza kwa watanzania upatikanaji wa mashamba ya kulima ngano mufindi. Akawaambia watu waelezwe wanaweza kuwekeza shilingi ngapi kulima ekari moja ya ngano. Akawaambia wawaite benki ya kilimo washirikishwe katika mpango huo au mabenki mengine. Akawashauri wawafuate wanunuzi wakubwa wa ngano kama bakhresa na azania na wengine ili washirikishwe na kuona wanawezaje kujicommit kwa soko la mazao yatakayovunwa.

Hii ndiyo tofauti ya Anthony.

Hiki alichokitoa ni business plan, ambayo iko workable, kwa sasa tunajua mataifa ya afrika mengi yananunua ngano kutoka Urusi na ukraine. Vita imefanya mazao haya yapande gharama sana.


Viongozi wa Afrika hakuna anayekuja na business plan kama hizi za kujiandaa kuchukua soko la hawa jamaa wanaopigana, utasikia viongozi wanapita na kuwaambia watu watumie vyakula kwa tahadhari, utasikia watu wanajustify kupanda gharama kwa ngano. Hawatazami fursa zinazotokana na migogoro hii.

road map ya Anthony ikifanya vizuri kwa kilimo cha ngano mufindi kuwatazama watumiaji wa ngano wakubwa ambao sasa katika kuwashirikisha watasema kama shida ni mvegu za ngano tulizonazo watasema, kama ni technolojia watasema, kama shida ni uzalishaji kidogo ndiyo sababu ya wao kuanza kuagiza nje watasema na yawezekana wakawekeana taratibu kuwa ili tununue kwenu tunahitaji mzalishe si chini ya kiwango hiki.

unaweza kuona yawezekana walikimbilia nje kwa sababu wakienda kutafuta ngano sokoni kununua kwa wakulima wanapata kidogo na hawajawahi kukutanishwa na wakulima ili wakulima wajue mahitaji ya hawa jamaa ni kiasi gani. Wazo la Anthony maana yake ni wakulima, wanunuzi, mabenki wanakutanishwa pamoja kuweka mipango ya pamoja na pengine kuwekeana malengo au target.

Only a blind man anaweza kultoa mfano wa ruzuku katika wazo kama hili.


kama mtu anaweza kulima ekari moja akapata milioni mbili faida ruzuku ya shilingi laki moja na nusu kwa ekari bila planning kama hii ya kuwaleta wadau pamoja kujadili a business plan ina maana gani?


weka hiyo ruzuku kwa mbolea bila mipango kama hii na itapita miaka 10 bado hawa ma giant wananunua ngano nje, sasa ni kitu gani unachokifanya?

mfano wako unaweka msisitizo kuwa wataalamu mara nyingi ni blind, wanashauri vitu ambavyo havileti tija ya kutosha kwenye jamii.
 
Back
Top Bottom