Mkuu wa mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka ameonya tabia ya watumishi wa umma wanaopanga ushuru mkubwa wakiwa wamekaa maofisini bila kujua shida wanayopata wawekezaji na kisha kumtaka kila mtumishi awekeze ama afanye biashara ili anapopanga ushuru ajue shida za walipa kodi kwa uhalisia .
Mtaka, wakati wa uzinduzi wa ofisi ya kituo cha uwekezaji kanda ya Nyasa mkoani Njombe amesema inaumiza mtumishi asie jua chochote kuhusu uwekezaji anakaa na kwenye kiti cha Serikali na kupanga ushuru mkubwa unaonyonya wakulima na kuishia kuua na kukimbiza wafanyabiashara na wawekezaji.
Awali Waziri wa nchi ofisi ya Rais Uwekezaji na Biashara, Prof Kitila mkumbo amesema alianza kuheshimu wawekezaji pale alipotumia mamilioni kuwekeza kwenye alizeti na kuishia kupata shilingi 600,000 na kisha kuwataka watungaji wa sheria na watekelezaji wa sheria za kodi kuwaheshimu wawekezaji kwasababu nchi haiendi bila wao na wanafanya kazi kubwa sana.