Antonio Guterres: Suala la Chanjo za kupambana na Corona lisichukuliwe kitaifa

Antonio Guterres: Suala la Chanjo za kupambana na Corona lisichukuliwe kitaifa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres amesema sio sahihi suala la chanjo dhidi ya Ugonjwa wa #COVID19 kuchukuliwa kitaifa

Katika ujumbe wake amesema, hakuna nchi itakayokuwa salama dhidi ya #CoronaVirus hadi nchi zote zitakapokuwa salama

Kauli yake inakuja baada ya nchi kadhaa zikiwemo Marekani, Uingereza na Urusi kuidhinisha chanjo za Pfizer/BioNTech, Moderna na Sputnik V ili kupambana na mlipuko huo

1609732249825.png
 
Sisi tuliwatangulia tukapiga ya kwetu ya nyungu. Nadhani kwasasa hili jambo liko kibiashara zaidi kila nchi inataka ije iuze chanjo yake ipige pesa.
 
Huo ugonjwa utatusumbua sana kwa sababu wakubwa wamejigawa jinsi ya kupambana nao yaani kila mtu kivyake na WHO hawana nguvu zaidi ya kutoa tamko tuu ambalo halina nguvu yeyote.
 
Ujumbe nimeuelewa, ila inabidi nikukosoe kwa sababu wewe si mtu wa kukosa umakini unapokuwa unaleta habari.

Maelezo yanataja mkurugenzi wa WHO, lakini kwenye picha kama reference maelezo ni ya Antonio Guterres ambaye ni katibu mkuu wa umoja wa mataifa. Kwa asiyefaham, atajua mkurugenzi wa WHO ni Antonio.
 
Back
Top Bottom