OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Your browser is not able to display this video.
Ni sahihi kwamba msemaji wa club ya Yanga bwana Antonio Nugaz hana hadhi ya kujadiliwa humu JF. Ila pale inapobidi ni lazima kufanya hivyo.
Binafsi nimekuwa nikimpuuza na kauli zake za hovyo na kudhalilisha club yake. Lakini hii ya kuita Mapinduzi Cup kwamba ni mashindano madogomadogo,siwezi kulipuuza.
Kauli hii imedhalilisha na kutusi mapinduzi tukufu ya Zanzibar na kutusi wazanzibar kwa ujumla.
Yanga wametoa tamko kujibaraguza kuonyesha kuheshimu Mapinduzi Cup,lakini wamefanya hivyo kwa kuchelewa. Kwani tayari msemaji wao ameshalikorogo.
Naamini waandaaji wa mapinduzi Cup watamtolea tamko huyu msemaji maandazi na timu yake,na kumtaka kufuta kauli hiyo.