Antonio Nugaz na ushauri toka kwa wake zake

Huyo jamaa anadhihirisha aina ya Watu ambao Yanga wanao. Mambo ya Yanga badala ya kuwauliza maboss zako wa Yanga useme nini, eti unaenda kuwauliza Wake zako Kitandani ni zaidi ya Ujuha aisee. Kwa kauli hii tu ilipaswa leo awe nje ya Yanga.
 
Kushauriwa ni kitu kimoja. Kufanyia kazi ushauri ni kitu kingine.

Kuchuja ushauri na kugundua pumba ziko wapi ni akili ya mtu binafsi.

Unaweza kushauriwa na mbuzi ukapata la maana. Ukashauriwa na Mfalme ikaws pumba.
Mbuzi?..🙄🙄🙄
 
Hapa lazima wazee wa Kamati ya ufundi wachungulie kwa uzuri,haiwezekani Utopolo watoe sare mfululizo, bora wangefungwa ingeleta mabadiliko kidogo. Utakuwa kuna mahali Haji Manara kawaendea pale Unguja, yaani Yanga iwe kituko.
Washambuliaji hatuna na pia nadhani kuna kitu humo ndani ila si wa nje hatufahamu kwani ule uchezaji wa mechi kadhaa pale katikati si huu wa sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Washambuliaji hatuna na pia nadhani kuna kitu humo ndani ila si wa nje hatufahamu kwani ule uchezaji wa mechi kadhaa pale katikati si huu wa sasa.

Hapo unakubaliana na dhana ya kwamba inawezekana kocha anahujumiwa?

Kwamba kuna watu wanaitaka hiyo nafasi.
 
Hakika usemalo Mkuu tungefungwa mechi zote hizo dawa ingepatikana na ndio sababu tulivyofungwa na Kagera kisha Azam baadae timu ilibadilika ikawa inacheza soka safi kabisa.

Hatuamini katika ushirikina Mkuu nionavyo kuna namna tu mule ndani kikubwa viongozi wakae waitatue angalau tupate matokeo na sio sare tu ambazo hazina faida yeyote zaidi ya kutukwamisha tu.
 
Hapo unakubaliana na dhana ya kwamba inawezekana kocha anahujumiwa?

Kwamba kuna watu wanaitaka hiyo nafasi.
Mmh!! Kwa hilo sidhani sababu mwanzo alipokuja Luc tulivurunda kama mechi kadhaa kocha alipokuwa mpya mpya na baadae kidogo tulipata matokeo na timu ilikuwa inacheza vizuri tu mbona.

Siamini kama ni hujma kwa Kocha Mtani.
 
Huu mwezi ni kama umewaangukia wenye wake wengi. Kila mtu na gear yake, at all its nonsense.
 
Mmh! Kwa hilo sidhani sababu mwanzo alipokuja Luc tulivurunda kama mechi kadhaa kocha alipokuwa mpya mpya na baadae kidogo tulipata matokeo na timu ilikuwa inacheza vizuri tu mbona.

Siamini kama ni hujma kwa Kocha Mtani.

Basi ndo ile nyota tuliyousema siku zile.

Huyu damu yake na yenu vimekataana, tafuteni suluhu mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…