Antony Grant Bloom. Myahudi mmoja mwenye akili kubwa sana

Joined
Oct 16, 2015
Posts
20
Reaction score
56
Wahuni wamembatiza jina la The Lizard akiwa kwenye meza ya poker, wanasema mwana ni cold-blooded na hii ndio sababu ya wao kumbatiza jina la Mjusi.

Antony Grant Bloom. Myahudi mmoja mwenye akili kubwa sana ya kiuchumi, ambaye ni Mjasiriamali, mchezaji kamari na mfanya ubashiri mkubwa sana pale Uingereza tangu enzi za ujana wake.

Tangu mwaka 2004 amepiga pesa nyingi sana, ameongoza mara 5 katika mara 7 za mashindano rasmi ya poker.

Mwaka 2009 alipata 75% ya umiliki wa Brighton akirithi nafasi ya Dick Knight pale Brighton & Hove Albion, timu ambayo aliipenda tangu akiwa na miaka 6.

Babu yake anayeitwa Harry alikuwa makamu mwenyekiti wa klabu miaka ya 1970, kwa hiyo kimahusiano, klabu ilikuwa ni familia.

Pauni 93m ni pesa iliyotosha kumfanya kuimiliki klabu, akaanza na upanuzi uwanja wa timu, Falmers stadium, ambao tunaufahamu kama American Express Stadium kwa sasa.

Miaka 7 Brighton wanapanda ligi kuu baada ya miaka 34.

Sasa moja kati ya sera ambazo Tony Bloom amezitengeneza Brighton hasa baada ya kupanda kwenye ligi ni kusajili wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa sana wa kucheza Premier League lakini kwa bei nafuu sana.

Wakifanikiwa kufanya vizuri timu inawauza na kupiga mshiko wa maana.

Juzi amesajiliwa Joao Pedro, baadae mtaona bei atakayopigwa, walimsajili Marc Cucurella kutoka Getafe kwa £15m, hakukaa misimu miwili wamemuuza £60m kwenda Chelsea.

Hao akina Moises Caicedo, Alexis Mac Allister, Yasin Ayari, Facundo Bounanotte, Kaoru Mitoma, Tariq Lamptey, Robert Sanchez na wengine kibao, wameenda hapo wakiwa wabichi, sio bahati mbaya ni sera ambayo Bloom na wenzake wameiweka.

Kinachofanyika ni kusajili wazoefu wachache tu, kijiji kisiishi bila wazee, lakini mipango yao ipo wazi.

Ndio maana nasema, hawa wadogo zetu kupotea ni ngumu. Mabomu ni mengi, muda wa kulipuka ndio bado.
FB_IMG_1684244053711.jpg
 
Ndio maana nasema, hawa wadogo zetu kupotea ni ngumu. Mabomu ni mengi, muda wa kulipuka ndio bado.View attachment 2624178
Kumbe

Msalimie Afisa Ubashiri mwenzetu
 
Back
Top Bottom