Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Peter Mavunde amegawa vifaa vya tehama vikiwemo kompyuta, printer Kwa shule zote za Serikali za jiji La Dodoma.
Sanjali na hayo, Mhe. Mavunde amegawa compyuta 41 kwa ofisi zote za kata katika jiji La Dodoma Pamoja na kuzindua jengo la maabara ya compyuta katika shule ya sekondari viwandani mara Baada ya kulifanyia uboresheaji.
Sambamba na hilo Mhe. Mavunde ameongoza zoezi la upandaji wa miti katika shule hio ikiwa ni ishara ya kuhimiza utunzaji wa mazingira.
wanafunzi wa shule ya sekondari Miyuji wamemshukuru Mhe Mavunde mara Baada ya kufanikishiwa upatikanaji wa vifaa hivyo vya tehama.