Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MONTAZA PALACE ALEXANDRIA 1988
Leo asubuhi nimeingia Maktaba na kukuta picha ya Montaza Palace.
Nilifika Montaza Palace kusali sala ya Ijumaa mwaka wa 1988 nilikuwa kwenye kozi mjini Akexandria na aliyenichukua alikuwa mmoja wa walimu zangu alipojua kuwa mimi ni Muislam.
Kozi ilikuwa na wanafunzi wengi kutoka Afrika lakini katika kundi zima lile Waislamu tulikuwa wawili tu.
Hii Montaza Palace lilikuwa jumba la Mfalme Farouk wa Misri la mapumziko yake wakati wa Kiangazi.
Montaza Palace baada ya mapinduzi ya mwaka wa 1952 Gamal Abdel Nasser aligeuza kuwa Kasri la Wananchi na kwa ajili hii msikiti uliokuwa ndani ya viwanja vya jengo hili ukawa wazi kwa watu kuja wakati wowote kusali
Niliikumbuka Montaza Palace na kushukuru kufika hapo baada ya kukisoma kitabu cha Mohamed Heykal, "The Road to Ramadan," alipokuwa akieleza Vita vya Yom Kippur mwaka 1973 wakati Misri na Syria zilipopigana na Israel.
Vita vilikuwa vinawaendea vizuri Waarabu na Anwar Sadat akaamua kuja Alexandria wakati vita bado vinauma.
Majeshi ya Misri yalikuwa yamevuka Suez Canal na kuingia Sinai na kuvunja Bar Lev Line mlima wa mchanga uliojengwa na Wayahudi kuzuia mashambulizi kutoka Misri baada ya Six Day War 1967.
Huyu Heykal mtu mwenye akili sana na akiheshimiwa mno Misri kwa ajili ya bongo lake.
Basi akaenda Alexandria kupata taarifa za vita kutoka kwa Commander in Chief mwenyewe na hivi ndivyo alivyojikuta uso kwa uso na Anwar Sadat ndani ya Montaza Palace.
Heykal mtu wa tasnifa sana.
Ukimsoma sharti utacheka.
Heykal anaeleza katika kitabu hicho kuwa, "Kwa muda Sadat aliniangalia bila ya kunijibu swali langu mkononi kashika glasi ya kinywaji chake hadi alipomaliza kunywa.
Alipomaliza kunywa akaniambia, "Heykal acha kunishughulisha na maswali yako madogo madogo mimi ni Mkuu wa Majeshi nashughulishwa na mambo makubwa.
Hayo mambo yako majibu ungeweza kupata Cairo."
Sasa Heykal anaanza kumkanyaga Sadat.
Heykal anasema Sadat akishughulishwa sana na muonekano wake kiasi kuwa uniform zake za Commander in Chief aliziagiza kutoka Paris na zilitoka kwa designer mkubwa sana duniani - Yves Saint Laurent.
Heykal bado anashindilia anasema, "Sadat alipokuwa kijana alitaka kuwa muigizaji lakini alikuwa hana kipaji hicho sasa alipokuja kuwa Rais zile camera za tv kwake yeye aliziona kama camera za Hollywood."
Huyu ndiye Mohamed Hasnain Heykal.
Hii picha ya Montaza Palace katika Maktaba imenikumbusha mengi.
photos.app.goo.gl

0 new items by Mohamed Said
photos.app.goo.gl