Mkuu
Moja ni Biceps na Triceps,
Pili ni vizuri kufanya mazoezi hayo kwa idadi maalumu na kwa interval mfano unapolala katika benchi na kuamua mufanya zoezi la kifua ukiwa na lengo la mfano mara 100,
hupaswi kunyanyua zote kwa awamu moja HATA KAMA UNA UWEZO HUO.
Kuna aina ya misuli(muscle) mwilini nikiwa na maana ya Type I na Type Ii(a and b), kuna ambayo huweza kustahimili kazi kubwa kwa muda mfupi na vice versa..Hivyo basiiwapo una lengo la kubeba mara 100(mfano) ni vizuri kubeba kwa awamu ya mara kumi kumi, yaani
Unalala unanyanyua mara kumi(KISHA unapumzika kwa dk mbili au tatu) na. kisha unaendelea kwa mzunguko huo.
Tatu, UZITO una maana sana..hii ni kwa sababu kwa mtu mwenye uzito wa kilogram 65(mfano) kutaka kubeba kilogram 45 au hamsini ni MATESO...Kwa kawaida mtu huanza kwa kubeba uzito mdogo na kuendelea kuongeza kadiri muda unavyokwenda.
Ni vizuri kukumbuka Physical exercise should be CHALLENGING but NOT DIFFICULT...
hii ikiwa na mana ya kuwa yasiwe mepesi saana ukapuuza lakini yasiwe magumu yakafanya ukachukia kufanya tena.