wa zion
JF-Expert Member
- Mar 23, 2013
- 223
- 481
Katika maisha kila mtu anapenda afanikiwe na kuweza kukidhi mahitaji yetu ya kila siku. Leo naongea na wewe ambae unawaza siwezi kufanya biashara sababu sina mtaji kwa kutoa uzoefu wangu mdogo kwenye biashara niliyoanza kiutani utani na nashukuru Mungu mambo sasa yanaenda vizuri kabisa.
Miezi michache iliyopita nilianza kuuza dagaa wa mwanza wa kukaanga na wakavu bila ya kutumia pesa yangu yoyote(NB: pesa nilikuwa nayo nilitaka kujaribu hili wazo langu) nilianzaje? kwa upande wangu ninaishi mwanza kwa sasa nikiwa sina ujuzi wowote wa biashara hii niliwatafuta wamama wanaouza dagaa wakavu nikawauliza bei ya dagaa wanayouzia nikakutanana na elfu 5 kwa sado nikamuita mama mmoja pembeni nikamwambia mimi nitakua nanunua kwako tu nataka bei ya jumla akaniambia dagaa wakavu jumla nitakuuzia 3500 kwa sado moja tukakubaliana nikapiga picha dagaa zake.
Nikachunguza bei ya dagaa wakavu Dar wanaoanikwa kwenye mawe, nikakutana na bei ya elfu nane kwa kilo moja dagaa wa kawaida tu nikaona itanilipa, kifupi niliingia facebook kule kuna makundi mengi ya wanawake wanasogoa tu nikatangaza biashara yangu kwa kuwambia kwamba ninakufikishia hadi mlangoni (nani asiependa hii raha ) nikawauzia 6500, unalipia kwanza kabla ya kupata mzigo wako (njia niliyotumia nyingine ni kuwafundisha wapi wanaweza kuuza dagaa watakao nunua kwangu mfano mama ntilie, masokoni)
Nikatafuta oda za dagaa wa kukaanga nikapata hii ilikua kwenye benki moja hapo mjini sikuwa na connection yoyote nilipost kwenye magroup ya whatsapp nikapata oda moja tu na huyo huyo mteja akaanza kunimiminia wateja wa kutosha, kukuza soko kwenye corporate industry nikampa ndugu yangu mmoja sample ya dagaa wa kukaanga(daraja la kwanza) nikamwambia sasa ingia kwenye maofisi ukifika wape waonje na tangaza soko lako na sasa si haba biashara inaenda vizuri.
vijana msio na ajira na mnaotoka vyuoni, tumieni vizuri mitandao ya kijamii na tafuta biashara kutokana na sehemu ulipo, si lazima uanze na pesa kubwa kuna biashara kauli unazotoa tu ndio biashara yenyewe