Anzisha biashara/mradi; panua biashara/mradi wako

Anzisha biashara/mradi; panua biashara/mradi wako

IPILIMO

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,819
Reaction score
801
Wana JF, Asilimia kubwa ya Watanzania hasa waishio mjini wanapenda kuanzisha miradi yao ya kiuchumi/Biashara za kiwango kidogo na cha kati.

Richa ya kupenda huko si wote wanaofanikiwa kuanzisha au wanao anzisha hawafikii malengo ya kibiashara. Biashara nyingi huanzishwa kwa KUIGA, kutokuwa na mfumo thabiti na wa kueleweka (biashara bubu), kuwa na mitaji midogo, kutokuwa na weledi wa kutosha katika kuendesha na kusimamia biashara husika, kutofanya tathimini na ufuatiliaji majini, kutofanya tafiti za kawaida za kimasoko nk.

Kampuni yetu imeshafanya Tathmini ya maendeleo ya biashara/miradi ya wateja kadhaa; asilimia 80 ya biashara hizo, zinaendeshwa bila kanuni za msingi za kibiashara; wengi wao kama ni ushauri wa haraka baada ya tathimini ni kuwa wazifunge au wahamishe eneo, au wabadili mfumo, au waongeze mtaji, au wabadili baadhi ya huduma/bidhaa nk. Wengi wao hata wenye muda wa miaka 5 katika biashara kiuhalisia hawajawahi kupata faida, na wala hawajui mtaji ni kiasi gani, wengine hawajui hata nini maana ya faida ktika biashara (they tend to ignore many business aspects kabla hawajafikia kuita profit- wengine hata mauzo tu huita faida). Hawafanyi mahesabu ya mtaji, ili kujua ukubwa wa mtaji walio nao kila baada ya muda fulani mfano kila baada ya miezi 6 nk.

Kwakweli biashara nyingi hasa za maduka pengine tunaziona ziko hai lakini kiuhalisia ziko hoi. Ikifika muda fulani kuanzia miaka 3 na kuendelea utaanza kuona kulegalega kwa biashara husika, mara leo imefungwa mara wiki, mwisho haipo. Akilazimisha basi inakuwepo tu lakini hakuna faida kwa mhusika, bali ni kuhudumia jamii tu ipate mahitaji yake.

Kama kampuni, tungependa kuwashauri wenzetu katika ujasiliamali, Kuwa na mradi/biashara maana yake ni kuwa Unahitaji kuwajibika kwa kiwango kikubwa, ujue kwamba umeanzisha kitu kinachohitaji Kukilea kama uleavyo mtoto; BIASHARA HUANZISHWA/HUZALIWA, HUKUA NA KUENDELEA (huku ikipanuka, sio kubaki na wazo lilelile la wakati wakuanzishwa miaka kadhaa nyuma) mfano kama mtu umeanzisha MGAHAWA malengo yako kama si kuwa na Hotel basi kuwa na modern restaurant, tena sio sehemu moja tu bali sehemu nyingi Tanzania, tena ukiongeza huduma ambatano mfano unaweza kubadili hata mfumo kutoka sole proprietor hadi kuwa kampuni ya catering nk.

Kwa leo ndo haya tu, sisi kama kampuni endapo unahisi unahitaji weledi zaidi katika kuhakikisha kuwa mradi/biashara yako inakuletea TIJA husika kama ilivyo malengo yako, sisi tutafanya hivyo; wasiliana nasi kwa huduma hizi za ushauri.
Baadhi ya kazi zetu ni kufanya uchambuzi wa mawazo ya miradi, kuandika maandiko ya miradi husika, kufanya tafiti za kimasoko na kutoa ripoti, kutrain wafanyakazi wa mradi, kutafuta uwezeshwaji wa kimtaji, kutafiti fursa za kiuwekezaji mahali tofauti tofauti nchini Tanzania, kufanya tathimini na ufuatiliaji wa mradi husika kisha kutoa ripoti, kutoa huduma za usimamizi wa miradi kama project managers (part time au full time nk).

Tutembelee na wasiliana nasi: KIMI DEVELOPMENT CONSULT LIMITED
Pia tutumie PM kwa mawasiliano zaidi.
 
mbona nyie hamtaki kufungua biashara ? mnatoa ushauri wa maneno matupu alafu sisi tuweke pesa zitoweke! wekeni na nyie pesa zenu kwa kuwa mnaushauri wa kuwpa watu mtakuwa mabilionea
 
mbona nyie hamtaki kufungua biashara ? mnatoa ushauri wa maneno matupu alafu sisi tuweke pesa zitoweke! wekeni na nyie pesa zenu kwa kuwa mnaushauri wa kuwpa watu mtakuwa mabilionea

Duh, tpmazembe INA maana huelewi kama na huu ni uwekezaji? biashara ni mambo mawili; kuuza bidhaa au huduma. Sisi ni kampuni tunafanya biashara ya kutoa huduma kwa wengine kama muuza bidhaa anavyouza bidhaa zake kwa watu nikiwemo Mimi na kampuni Yetu. Tumewekeza rasilimali zetu ktk biashara hii. Nadhani umenielewa.
 
Back
Top Bottom