ANZISHENI TIMU ZENU!

ANZISHENI TIMU ZENU!

BatteryLow

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2011
Posts
446
Reaction score
149
Nimefurahia sana Serikali kuwapiga 'stop' wafanyabiashara wanaonyemelea kuwekeza kwenye vilabu vikubwa vya soka Tz, Yanga na Simba.
Ushauri wangu kwa hili ni kuwataka wafanyabiashara hawa kuanzisha vilabu vyao kama alivyofanya mwenzao kwa kuanzisha Azam na ikawa moja ya timu zinazofanya vizuri ktk ligi kuu.
Uanzishwaji wa timu nyingine pia utazidisha ushindani ktk ligi soka Tz hivyo kuinua kiwango cha soka nchini tofauti na kung'ang'ania kwenye timu zile zile za zamani.
Huo ni ushauri wangu tu!!
 
Hivi Roman Abrahamovich angefanyiwa hivi chelsea ingekua pale ??
 
Ubinafsi wa watanzania chanzo cha umaskini na fitina, timu zibinafisishwe kwa masharti mazuri ili soka likue na matunda tutayaona mbeleni, kwani timu km Yanga ikimilikiwa na Manji halafu ikawa na mafanikio kitaifa na kimataifa we shabiki una hasara gani????
 
Kuna timu nyingi zinakwama kwakukosa wawezeshaji.
 
We ni pimbi sana tu,wafanya biashara wanatafuta faida ya haraka,hawezi kwenda kuwekeza sehemu isiyo na faida,aanzishe timu wakati wenye timu ndio wanao taka hao mo na manji wawekeze hapo,isitoshe wanajitolea tu km wanachama hapo wanahangaika km wewe mnataka nini? Kwani wamesema wakiwekeza watapeleka timu hizi India? Zitabaki k'koo daima.
 
Ubinafsi wa watanzania chanzo cha umaskini na fitina, timu zibinafisishwe kwa masharti mazuri ili soka likue na matunda tutayaona mbeleni, kwani timu km Yanga ikimilikiwa na Manji halafu ikawa na mafanikio kitaifa na kimataifa we shabiki una hasara gani????
Ok, uko vizuri, lakini labda mm sielewi tofauti ya ku-binafsisha na ku-wekeza.
 
Wewe una Mawenge Kweli!!! Hivi Kule Ulaya Timu Walikowapa Wawekezaji wa Kichina, Kiarabu na Wamerekani Hawajui Mpira au??
 
Nimefurahia sana Serikali kuwapiga 'stop' wafanyabiashara wanaonyemelea kuwekeza kwenye vilabu vikubwa vya soka Tz, Yanga na Simba.
Ushauri wangu kwa hili ni kuwataka wafanyabiashara hawa kuanzisha vilabu vyao kama alivyofanya mwenzao kwa kuanzisha Azam na ikawa moja ya timu zinazofanya vizuri ktk ligi kuu.
Uanzishwaji wa timu nyingine pia utazidisha ushindani ktk ligi soka Tz hivyo kuinua kiwango cha soka nchini tofauti na kung'ang'ania kwenye timu zile zile za zamani.
Huo ni ushauri wangu tu!!
Ushindwe na ulegee
 
Ubinafsi wa watanzania chanzo cha umaskini na fitina, timu zibinafisishwe kwa masharti mazuri ili soka likue na matunda tutayaona mbeleni, kwani timu km Yanga ikimilikiwa na Manji halafu ikawa na mafanikio kitaifa na kimataifa we shabiki una hasara gani????

Wengine siyo mashabiki tu, ni wanachama...halafu, unajuaje kwamba huyo unayemtaja anaweza kuleta mafanikio???? Kingine, katiba ya YANGA hairuhusu ukodishwaji....katiba inaruhusu uanzishwaji wa kampuni inayomilikiwa na YANGA (yaani klabu na wanachama wake) na siyo na mtu mmoja....Akitaka ukodishwaji wanachamas waelimishwe na kuambiwa uzuri na ubaya wa kukodishwa...halafu wanachama hao waambiwe kilichokwamisha uanzishwaji wa kampuni.....
 
Back
Top Bottom